TAKRIBAN wiki moja baada ya kumaliza eda tangu alipofariki mumewe
Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari 2, mwaka huu, staa mkubwa wa filamu za
Kibongo, Wastara Juma anagombewa na midume ikitaka kumuoa.
Akizungumza na mwandishi wetu akiwa nchini Oman,
Wastara alifunguka kuwa tangu amalize eda yake hiyo amekuwa akipata
usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume mitandaoni na wanaomtamkia mwenyewe.
“Jamani
mpaka nahisi kuchanganyikiwa kabisa, wanaume zaidi ya mia tano hata
sijui walipotokea wanataka kunioa, hadi nahisi majanga,” alisema
Wastara.
Wastara alisema kuwa wanaume hao wamekuwa wakihangaika bure
kwa sababu kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa kwani anapotembea bado
anasikia harufu ya mumewe Sajuki.
“Bado harufu ya Sajuki ipo mwilini
mwangu, wanaume wanaonitolea macho mtoto wa mwenzao wanakosea sana,
sifikirii kabisa suala hilo kwa sasa,” alisema Wastara mwenye mtoto
mdogo aliyezaa na Sajuki.
0 comments:
Post a Comment