MWANAUME mmoja aliyefahamika kwa
jina la Ezekiel Malika 'Baba Kulwa' amenaswa gesti na mkewe akiserebuka
na shoga aitwaye Aunt Steve na kuibua mtiti mzito..
Tukio hilo lilivuta umati lilijiri Mei 20, mwaka huu kwenye gesti
moja iliyopo Mwananyamala, Dar ambapo mke wa Ezekiel
alivamia na kutembeza mkong’oto wa hasira kwa mumewe.
Mei 19, mwaka huu, saa 3:15 asubuhi, mwanamke mmoja
ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya heshima yake mtaani
alilipigia simu gazeti hili na kutoa malalamiko kwamba mumewe amekuwa na
tabia ya kulala na wanaume wenzake ambao ni mashoga.
“Jamani, mimi
naitwa… (akataja jina), naomba jina langu lisiandikwe .
Malalamiko yangu ni kwamba, mume wangu amekuwa na tabia ya kulala na
mashoga, hivi ninavyoongea ana ahadi ya kukutana na mmoja wao gesti kama
si kesho basi keshokutwa, niliona meseji kwenye simu ya mume wangu.
“Nawaomba chondechonde, mnisaidie ili hii tabia ikome. Nipo tayari
kusikia maelekezo yenu ,” alisema kwa masikitiko mwanamke
huyo.
Mratibu wa Oparesheni hii alimpa
maelekezo mwanamke huyo akimtaka kufuatilia kwenye simu ya mumewe ili
kubaini siku ya wawili hao kukutana gesti.
“Nawaahidi kwamba leo
hiihii kabla giza halijaingia nitakuwa nimejua siku yao ya kukutana,
naomba msiache kupokea simu yangu jamani.”
Saa 11:00 jioni, mwanamke huyo alipiga simu tena na kupokelewa na yuleyule mratibu wake aliyempa maelekezo.
Mwanamke: Mchana wakati mume wangu amekwenda kuoga niliipekua simu yake, wanakutana kesho kwenye gesti ya …(anaitaja jina).
“Kwa hiyo mtanisaidiaje?”
“Kwa hiyo mtanisaidiaje?”
OFM: Wewe kuwa beneti na mumeo, kesho akiondoka na wewe ondoka hata kwa
kujificha, mfuatilie hadi kwenye hiyo gesti huku ukitupa mawasiliano.
Mwanamke: Hilo halina shida, nitakodi Bajaj halafu nitawaambia.
OFM: Oke, kuwa makini, mawasiliano ni muhimu. Tutawanasa kisha wakaishie polisi.
Mwanamke: Nitashukuru sana jamani. Loo! Kweli dunia imekwisha, mwanaume
ana mke, hatosheki anatafuta wanaume wenzake, afadhali angekwenda kwa
machangudoa.”
Siku ya tukio saa 8:00 mchana, mwanamke huyo akiwa ameongozana na mashoga zake, walifika kwenye gesti hiyo na kubana sehemu ambayo wangeweza kumwona anayeingia na kutoka kisha akawasiliana na mratibu wa OFM ambaye aliwatuma wapekuzi watatu wenye kamera za kupiga picha kwa umbali wa mita 100.
Kufumba
na kufumbua, Aunt Steve aliwasili na kuzama ndani ya gesti hiyo kwa
kutumia mlango wa nyuma ili asionekane kwa vile sheria ya serikali
kuhusu gesti, wanaume hawaruhusiwi kuingia kwenye chumba kimoja.
wapekuzi wetu wakiwa tayaritayari walitega katika pembe tatu za gesti hiyo ili kunasa tukio hilo hatua kwa hatua.
Kufumba na kufumbua, Baba Kulwa alitokea na kuingia ndani ya gesti hiyo kwa kutumia mlango mkubwa wa mbele huku akiwa hajui kama arobaini yake ilikuwa imebakiza dakika chache siku hiyo.
Alifika mapokezi na kupewa chumba No. 01, akaenda uani na
kufanya jitihada kubwa za kumpitisha shoga huyo kwa mlango wa nyuma hadi
ndani.
Baada ya wote kuzama chumbani, mke
wa mwanaume huyo, mashosti zake na wapekuzi waliwaacha kwa dakika kumi
ili wafikie hatua ya kuchojoa nguo hivyo kuweza kuwanasa wakiwa watupu.
Baada ya dakika kumi, wafumaniaji wote walizama ndani na kugonga mlango wa chumba walichomo wawili hao huku shosti mmoja wa mwanamke huyo akijitambulisha yeye ni mhudumu anawaongeza taulo. Baba Kulwa bila kufahamu janja hiyo alifungua mlango kidogo na kuchomoza kichwa lakini ghafl a akinadada hao akiwemo mkewe walimvamia na kusukuma mlango, wakazama ndani.
Wawili hao walikutwa hawana nguo, ndipo msala ulipomwangukia Baba Kulwa na Aunt Steve wake, mke akipewa nguvu na wapambe wake waliwatembezea kipigo huku wakiwakejeli kwa tukio hilo la aibu.
Baada ya kuwaweka wote chini ya ulinzi, waliwatoa nje huku Baba Kulwa akiomba msamaha kwa mkewe lakini bila kukubaliwa.
“Msamaha wa nini? We si kidume cha kweli, twendeni nje tukawaanike mbele ya watu,” alisema mwanamke huyo.
Katika hali iliyoonekana ni kukosa
umakini wa kuweka kizuizi vizuri, Aunt Steve alifanikiwa kuchoropoka
kama samaki aina ya kambale na kutokomea kusikojulikana huku wanawake
hao wakimsindikiza na zomeazomea hadi wakafunga mtaa.
GPL
0 comments:
Post a Comment