ndo kwa mwanamuzi huyo.
Akizungumza na JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Morogoro juzi saa 1:45 usiku dereva huyo wa gari maalumu la kubebea maiti kutoka kampuni ya Nuru Funeral Servise ya jijini Dar es Salaam, Narasco Robert alisema kuwa alilazimika kuwakwema mashabiki hao baada ya kulizingira gari lake na kumtaka azime gari ili wapate nafasi ya kulisukuma mwanzo wa mji hadi mwisho wa mji huo.
Robert alisema kuwa baada ya kuona kundi kubwa la vijana hao alilazimika kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake na kuongeza mwendo na kuwaacha vijana hao na kusubiri msafara mbele kufuatia kuwaacha mbali.
Msafara huo uliwasili katika mji huo majira ya saa 4:45 jioni wakati ukitokea jijini Dar es Salaam ambapo katika miji midogo ya Mkambarani, Kinglwira NaneNane kulijaa umati wa watu kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro wakipunga mikononi na kuonyesha ishara ya vidole viwili ikiwa ishara ya kuonyesha upendo kwa mwanamuziki huo.
Umati huo wa mashabiki uliongezeka mara dufu baada ya kuwasiri eneo la Msamvu hadi stendi ya Dodoma huku kundi lingine likianzia barabara ya Mazimbu Kihonda hadi nyumbani kwa mama mzazi wa Mangwea ambapo ulifika majira ya saa 12:15 jioni.
Baada ya familia ya karibu kuutambua mwili wa marehemu Albert Mangwea, mwili huo uliondolewa na kwenda hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ambapo askari wa jeshi la polisi waliongoza msafara huo hadi chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.
Licha ya watu wa rika mbalimbali kujitokeza kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro adha kubwa iliwakuta watumiaji wengine baada ya kuwepo kwa msongomano wa magari yaliyokuwa yakijaribu kuupita msafara huo na kuziba magari yaliyokuwa yakitoka Morogoro kwenda Dar es Salaam huku waendesha pikipiki maarufu bodaboda nao wakionekana kuwa chanzo cha vurugu katika msafara huo hasa kwa tabia ya kuendehsa pikipiki hizo kuvunja sheria za usalama wa barabarani.
0 comments:
Post a Comment