Lwakatare (anayeonyesha alama ya V) na mfuasi wake mahakamani.
DAR ES SALAAM.
MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP) amezidi kumng’ang’ania Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare (pichani) baada ya kuanza mchakato wa kupinga dhamana yake.

Lwakatare, ambaye anakabiliwa na kesi ya jinai
pamoja na mwenzake Ludovick Joseph Rwezaura katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, aliachiwa huru kwa dhamana Juni 11, mwaka huu, baada ya
kusota rumande kwa mie
zi miwili na siku 23.
zi miwili na siku 23.
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Aloyce Katema
anayesikiliza kesi hiyo,alimwachia huru kwa dhamana Lwakatare, baada ya
Mahakama Kuu, Dar es Salaam kuwafutia mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa
yakiwabili.
Hata hivyo DPP amewasilisha katika Mahakama ya
Kisutu taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama Kuu, kupinga
uamuzi wa Mahakama ya Kisutu kumpa dhamana.
Mbali na taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa kupinga dhamana yake, DPP pia tayari ameshawasilisha katika Mahakama ya Rufani, maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuwafutia mashtaka ya ugaidi.

Katika maombi hayo, DPP anaiomba mahakama hiyo
iitishe majalada ya kesi hiyo na kuchunguza uhalali wa uamuzi wa
Mahakama Kuu, uliotolewa na Jaji Lawrence Kaduri, kuwafutia washtakiwa
hao mashtaka ya ugaidi.
Anadai kuwa katika hati ya maombi ya washtakiwa
hao waliyowasilisha Mahakama Kuu, hapakuwapo na maombi ya kufuta
mashtaka, na kwamba hapakuwa na taarifa zilizowasilishwa dhidi ya
washtakiwa ambazo Mahakama Kuu ingezingatia katika kuamua kama ni halali
au la.
Hata hivyo Lwakatare kupitia wakili wake, Peter Kibatala kwa niaba ya jopo la mawakili wenzake, amewasilisha pingamizi la awali dhidi ya maombi hayo, akianisha hoja mbili, ambazo mawakili wake watazitoa wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo.

Anadai kuwa maombi hayo ya marejeo yana dosari
ambazo haziwezi kurekebishwa kutokana na kushindwa kuambatanisha nakala
ya mwenendo wa uamuzi unaolalamikiwa ambao ndiyo maombi hayo yamejengwa
na kwamba kiapo kinachounga mkono maombi hayo kimehusisha mambo mengine
yasiyohusika.
Kabla ya kufutiwa mashtaka ya ugaidi washtakiwa
hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne, matatu kati yake yakiwa ya
ugaidi na moja la kawaida la jinai, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, wakidaiwa kula njama na kupanga kumteka Mhariri wa gazeti la
Mwananchi Dennis Msacky na kisha kumdhuru kwa kutumia sumu.
Walipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa mara
ya kwanza, Machi 18, mwaka huu na kusomewa mashtaka hayo na kukana
baada ya kutakiwa na mahakama hiyo kujibu,licha ya kwamba hawakutakiwa
kujibu chochote kwa kuwa mashtaka hayo husikilizwa na Mahakama Kuu tu.
Kutokana na mazingira hayo, mawakili wake
walimwombea dhamana, lakini siku ambayo Hakimu Emillius Mchauru
alitarajia kutoa uamuzi wa maombi hayo ya dhamana, DPP aliwasilisha hati
ta kuwafutia mashtaka. chanzo mwananchi
0 comments:
Post a Comment