MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Moshi, mkoani
Kilimanjaro imewahukumu raia wawili wa Kenya na mwanamke mmoja Mtanzania
jela miaka 67 baada ya kupatikana na hatia ya kula njama na kupora Sh
milioni 239 kutoka benki ya NMB tawi la Mwanga, Kilimanjaro.
Uporaji huo ulifanyika Julai 11,2007
ambapo pia watu hao waliiba bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) mali
ya Jeshi la Polisi nchini, na kumuua askari Polisi Michael Milanzi
aliyekuwa lindo.
Watuhumiwa hao waliofungwa ni Samweli
Git
au maarufu kwa jina la Saitoti na Michael Joseph Kimani (wote kutoka
Kenya) na Mtanzania Elizabeth Elias maarufu kwa jina la Bella mkazi wa
Kwangulelo mkoani Arusha.
Jopo la makakimu watatu wakiongozwa na
Panterine Kente liliwahukumu kwenda jela miaka saba kwa kosa la kwanza
ambalo ni kula njama; miaka 30 kila mmoja kwa kosa la uporaji pamoja na
miaka 30 kwa kosa la wizi wa silaha.
Hakimu huyo alisema kuwa adhabu hizo
zinaenda pamoja hivyo washitakiwa watatumikia kifungo cha miaka 67 jela,
mbali na hukumu hiyo Mahakama hiyo pia iliwaachia huru ndugu watatu ni
ambao ni Devotha Elias Masenza, Ntibasana Elias Masenza na Julian Elias
Masenza na mtu mwingine Calist Kanje baada ya ushahidi dhidi yao
kushindwa kuishawishi Mahakama.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo , wakili wa
Serikali Tamali Mndeme aliomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa
washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda
makosa kama hayo. CHANZO HABARILEO.
0 comments:
Post a Comment