PICHA ZIKIMUONYESHA MUME WA JOYCE KIRIA NA VIJANA WENGINE WA CHADEMA WAKIWA NA PINGU WAKIKABILIWA NA KESI DHIDI YA UGAIDI IGUNGA HUKU POLISI NAO WAKIMKEMEA JOYCE KIRIA.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.
Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.Kamanda Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013.
POLISI WAMKEMEA JOYCE KIRIA,HAYA HAPA NDIO MAJIBU.INASIKITISHA kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na
kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani
analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu
akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai.
Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika
kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu (Imetolewa na Advera Senso
Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania).Joyce Kiria akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo alidai hajui mume wake yuko wapi.
0 comments:
Post a Comment