Katibu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na
vijana wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu
mkazi Tabora mjini.
Mbali ya
Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni Evodius Justinian wa Buboka, Oscar
Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel Kihawa
wa Dodoma, leo wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na kumwagia
tindikali Musa Tesha katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga
uliofanyika mwaka 2011.
Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.
Kesi hiyo
ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, ya
Tabora Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na
Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara Baada ya kusomewa shitaka
hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili Prof Abdalah Safari,
ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela ulitoa hoja kuiomba
mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa sababu, kwanza mashtaka
hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa
Mashtaka nchini.
Sheria za
uendeshaji wa makosa kama hayo hapa nchini zinadai kuwa mashataka kama
hayo yanapofunguliwa ni lazima ridhaa ya Mkurugenzi wa mashtaka iwepo.
Kwa kuwa ridhaa hiyo haikuwepo, mawakili waliiomba mawakili kuitupilia
mbali kesi hiyo.
Sababu ya
pili iliyotolewa na upande wa Utetezi ilikuwa kwamba maelezo ya kesi
kuwa ni ya ugaidi, yalikuwa hayaonyeshi kuwa ni ya kigaidi tofauti na
makosa mengine ya kawaida kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hivyo
waliiomba Mahakama kutupilia mbali shitaka hilo au lifunguliwe kama kosa
la kawaida.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment