Mchezaji wa timu ya soka ya wakuu wa wilaya nchini, Herman kapufi kulia akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa Sua Vteran Francis Kwetukia kushoto wakati wa mchezo wa kirafi wa wakuu hao wa kujipima nguvu kabla ya kucheza na wabunge katika mchezo wa kuchangia fedha kwa ajili ya ujen
zi wa kituo maalum cha walemavu wa ngozi (Albino) kitakachonjengwa Arusha, ambapo katika mchezo huo ulimalizika kwa Sua Veteran kuibuka na ushindi wa bao 5-2 katika uwanja wa jamhuri Morogoro.Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya soka ya wakuu wa wilaya nchini imeanza vibaya katika michezo ya kujipima nguvu dhidi wapinzani wao ya timu ya wabunge baada ya kukubali kipigo cha kutandikwa bao 5-2 dhidi ya Sua Veteran katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.
Kamwe timu ya wakuu wa wilaya hataitaweza kumsahau mshambuliaji hatari wa timu ya Sua Veteran, Fikiri Hussein (Mmachinga) aliyekuwa mwiba mchungu baada ya kuonekana shujaa kwa kufunga bao nne pekee yake baada ya kazi nzuri za Hamis Machuna aliyetoa pasi moja ya goli na pasi tatu zikitolewa na Ally Bushir huku bao la la tano likikwamishwa kimiani na mshambuliaji Faustine Maerere akipokea pasi ya Ally Bushiri.
Washambuliaji, Chriatian Meela na Paul Mzindikaya ndiyo walioifutia aibu timu ya wakuu wa wilaya ya kufunga bao hizo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Sua Veteran kuibuka na ushindi wa bao 5-2.
Akizungumzia maandalizi ya michezo wao dhidi ya wabunge, Mwenyekiti wa micheza kwa wakuu wa wilaya nchini, Venance Mwamoto alisema kuwa maandalizi yao ya timu zao za soka na netiboli yanaenda vizuri kwani kwa sasa wapo katika mazoezi makali na wana imani ndani ya wiki mbili zitatosha vijana wake kuimarika na kutoa ushindani wa hali ya juu kabla ya kuvaana na wapinzania katika michezo ya kuchangia fedha kwa ajili ya kituo cha ujenzi wa walemavu wa ngozi (Albino).
Mwamoto alisema kuwa katika mchezo wao wa kwanza wamepoteza dhidi ya Sua Veteran kwa kutandikwa bao 5-2 lakini katika michezo ijayo ya kirafiki ambayo wanatarajia kucheza na Pwapwa Veteran n watajitahidi kurekebisha kasoro zilizojitokeza ili mchezo huo kuibuka na ushindi.
Kambi ya timu za soka na netiboli imevunjwa rasmi Manispaa ya Morogoro na kuelekea Dodoma ambako wataweka kambi kabla ya michezo hiyo kutokana na sababu ya kutaka kuhudhuria kikao cha wakuu wa mikoa na wilaya ambacho kitafanyika mkoani Dodoma kuanzia leo (Jumatatu) na wakiwa huko timu ya netiboli itajipia ubavu na dhidi ya timu tatu tofauti za CCM, CBI na Tamisemi.
0 comments:
Post a Comment