Mkuu wa Chuo cha Ujenzi Morogoro Mhandisi, John Mdee kushoto akifafanua jambo kwa Naibu Meya wa Manispaa yaMorogoro, Lidya Mbiaji kulia wakati Naibu huyo alipofanya ziara ya kukitembelea chuo hicho na kufunga mafunzo yamafundisanifu na mafundistadi wa fani za barabara, majengo na magari chuoni hapo, hivi karibuni.
MANISPAA ya Morogoro imeonekana kuvamiwa na makundi ya watu pamoja na vichocheo mbalimbali vinavyosababisha ongezeko la maambukizi ya Ukimwi ndani ya Manispaa hiyo ikiwemo suala ya usagaji na watu kufanya ngono kinyume na maumbile hasa kushamili vyuoni.
Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Lidya Mbiaji alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya siku moja juu ya maambukizi ya vir
usi vya Ukimwi kwa waandishi hao na kusema kuwa vichocheo hivyo vimeonekana kushamili vyuoni ambapo vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na masuala hayo kwa lengo la kujipatia Fedha.
Mbiaji ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya kudhiibiti Ukimwi katika baraza la madiwani alisema kuwa kamati yake ilifanya utafiti na kugundua kuwa sehemu za vyuoni kumekuwa na maambukizi hayo kutokana na wanafunzi wengi kufanya ngono hizo ikiwa ni wao kwa wao ama kwa wtu wengine wanaowazunguka.
Aidha alisema kuwa maambukizi ya Ukimwi kwa Manispaa ya Morogoro yameongezeka kwa kasi ukilinganisha na awali ambapo alisema takwimu kwa mwaka 2007-2008 maambukizi yalikuwa 6.5, ambapo kwa mwaka 2010 hadi desemba 2012 takwimu zimeonyesha kufikia asilimia 10.2 jambo ambalo limekuwa ni tishio
“Hali ya maambukizi mapya kwa Manispaa yetu imezidi kuwa mbaya na inaongezeka kila mara, mpaka wanafunzi wetu wa shule za msingi na sekondari wanapata maambukizi, sasa nadhani juhudi za maksudi zinatakiwa kuchukuliwa,”alisema Naibu Meya huyo.
Pia aliyaomba madhehebu ya dini kuendelea kusaidia katika kukemea suala la watu kufanya ngono kwa jinsia moja na hata kutembelea vyuoni ,pamoja na katika shule za msingi na sekondari na kuonyesha masikitiko yake kwa kuonekana maambukizi kuwa mengi hasa kwa watoto wa kike.
Kwa upande wake Mratibu wa Ukimwi Manispaa hiyo Dk Getruda Lebby alisema kumekuwa na tabia hatarishi na vichocheo vingi vinavyosababisha kuongezeka kwa maambukizi ikiwa ni pamoja na kuwapo kwa ngoma za usiku maarufu kama vigodoro,kunema mwari.
Dk Lebby alitaja vichocheo vingine ni Minada, semina na makongamano, maonyesho mbalimbali yakiwemo ya kitaifa,kuwapo kwa vituo vya michezo na wafanyabiashara wanaokuja kufuata bidhaa mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment