Zitto Kabwe amefunguka na kudai kuwa kwa sasa wanajiandaa
kufanya mapinduzi ya nchi endapo serikali watu walioficha
mabilioni uswiswi hawatashughulikiwa ipasavyo.
Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha
nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji
vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo
inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa
Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa
kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha
ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge.Zitto Kabwe anatoa angalizo katika hatua hiyo ya jaji Werema kwa kusema kuwa hatua hii isiwe "zima moto" na daganya toto ili kuwafumba macho watanzania.
Ubabaishaji wowote kwa mujibu wa Zitto Kabwe utasababisha mapinduzi ya nchi.....
Hii ni post yake aliyoweka katika mtandao wa twitter
0 comments:
Post a Comment