Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Mwanamuziki Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA,
amepata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady
Jay Dee, baada ya kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti
ambao ndani yake
kuna jina la Jay Dee.
Tofauti na ilivyozooeleka katika wimbo wa Mabinti,
kwa mara ya kwanza Mwana FA aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee
‘Anaconda’, hali iliyowafanya mashabiki wamtake arudie tena na kutenda
haki.
Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua
kurudia wimbo huo na alipofika katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba
kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na
mashabiki kumtaka arudie tena na tena.
Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi
na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana,
lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Awali shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400
tu. Lakini mpaka inafika saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa
kwa shoo hiyo watu waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.
CHANZO THE CHOICE.
0 comments:
Post a Comment