Na Mahmoud Zubeiry.
IVORY
Coast imefanikiwa kusonga hatua ya pili na ya mwisho katika kuwanai
tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia, baada ya kuifunga Tanzania
mabao 4-2 jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa
Kundi C kanda ya Afrika.
Kwa
ushindi huo, Ivory Coast imetimiza pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa
na timu nyingine yoyote katika kundi hilo na sasa itasubiri kucheza na
mmoja wa washindi weng
ine wa makundi mengine tisa ili kuwania kwenda
Brazil mwakani.
Tanzania
inabaki na pointi zake sita, huu ukiwa mchezo wa kwanza kufungwa
nyumbani katika kampeni hizi na Morocco bila kuhusisha matokeo yake na
Gambo, ina pointi tano.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Mehdi Abid aliyesaidiwa na Hamza
Hammou, Bauabdallah Omar wote kutoka Algeria, hadi mapumziko Ivory Coast
tayari walikuwa mbele kwa mabao 3-2.
Stars
ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao mfungaji Amri Ramadhani Kiemba
dakika ya kwanza tu aliyepokea pasi ya Mbwana Ally Samatta kufuatia
mpira wa kurushwa na Erasto Edward Nyoni kusababisha kizazaa langoni mwa
Tembo wa Abidjan.
Nyoni
alirusha kama amepiga kwa mguu karibu kabisa na kibendera cha kona
kufuatia beki Suleiman Bamba kumpitia Thomas Ulimwengu na kutoa nje na
mpira ukaokolewa kabla ya kumkuta Samatta aliyempelekea mfungaji.
Ivory
Coast wakasawazisha bao hilo dakika ya 15 kupitia kwa Lacina Traore
baada ya mabeki wa Stars kuzembea kuokoa na Yaya Toure akafunga la pili
kwa mpira wa adhabu dakika ya 23, nje kidogo ya eneo la hatari.
Bao hilo lilitokana na wachezaji wa Stars kupanga ukuta wao vibaya na kumpoteza maboya kipa wao, Juma Kaseja.
Stars
ilirudi mchezoni na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 35
mfungaji Ulimwengu aliyeunganisha krosi maridadi ya Shomary Kapombe.
Hata
hivyo, Ivory Coast wakapata penalti rahisi baada ya Gervinho
kujiangusha wakati anakabiliana na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Yaya Toure
akaenda kumtungua Kaseja dakika ya 43.
Kipindi
cha pili Stars ilikianza vizuri na kushambulia mara nyingi langoni mwa
Ivory Coast, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi.
Mabadiliko
yaliyofanywa na kocha Mdenmark, Kim Poulsen dakika ya 87 kumtoa kiungo
Mwinyi Kazimoto na kumuingiza mshambuliaji Vincent Barnabas yaliigharimu
Tanzania kwa kufungwa bao la nne na kupotea kabisa mchezoni.
Baada
ya kutoka Kazimoto, aliyetekeleza majukumu yake vizuri leo, Ivory Coast
wakatawala sehemu ya kiungo na kutengeneza bao la nne lililofungwa na
Bonny Wilfred dakika ya 88.
Pamoja na kufungwa, Stars ilicheza soka safi ya kuvutia na mabao yote yalitokana na makosa – na si kuzidiwa uwezo.
Kikosi
cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomary
Kapombe/Khamis Mcha dk 85, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank
Domayo, Mwinyi Kazimoto/Vincent Barnabas dk 87, Salum Abubakar, Thomas
Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba.
Ivory
Coast; Boubakar Barry, Arthur Boca, Didier Zakora, Solomon Kalou/Sio
Giovanni, Gervais Yao, Jean Jarques Gosso Gosso, Alain Aurier, Lacina
Traore/Bonny Wilfred, Yaya Toure, Geoffrey Serey na Suleiman Bamba/Nori
Koffi Christian.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MICHUANO YA KUSAKA TIKETI YA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA TANZANIA 2 IVORY COAST 4.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment