BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSHAMBULIAJI JUMA BANGUKE AIVUSHA TIMU YA MZINGA KWA KUFUNGA BAO 4-0 DHIDI YA SABASABA MASHINDANO YA TIKA CUP 2013.

 MLINDA Mlango wa Gereji Fikiri Nassouro akiondosha hatari ikiwa moja ya hekaheka iliyoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa nane Bora mtoani katika mashindano ya TIKA CUP 2013 Manispaa ya Morogoro katika uwanja wa Shujaa mkoani hapa, katika mchezo huo Kihonda ilikub
ali kipigo cha bao 1-0.
PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
 MSHAMBULIAJI KATA YA KIHONDA, CHALANGWE MFAUME AKITAFUTA MBINU YA KUWATOKA WALINZI WA GEREJI KATIKA MCHEZO HUO.
KUSHOTO NI SHABIKI WA MSAMVU TERMINAL AKIKUNJA NGUMU NA KUMTANDIKA SHABIKI WA TIMU YA MWEMBESONGO KUFUATIA KUTOFAUTIANA JAMBO BAADA YA TERMINAL KUTANDIKWA BAO 10-9 KWA NJIA YA MIKWAJU YA PENALTI BAADA YA KUFUNGA BAO 1-1 KATIKA DAKIKA 90.


Na Juma Mtanda, Morogoro.
MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya kata ya Mzinga, Juma Banguke amefanikiwa kupachika mabao 4 nyavuni wakati timu yake ikichuana na Sabasaba katika mchezo mkali wa hatua ya nane bora mtoani mashindano ya TIKA CUP 2013 Manispaa ya Morogoro na kuivusha kucheza ligi ya kutafuta bingwa wa mashindano hayo kufuatia kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-0 uliofanyika uwanja wa Kilakala Makaburini mkoani Morogoro. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa Mwenyekiti wa mashindano ya TIKA CUP 2013 Manispaa ya Morogoro, Msifuni Chenjela alisema kuwa timu ya Mzinga imeungana na timu nyinge tatu kucheza ligi ndogo ya kusaka bingwa mashindano hayo baada ya mshambuliaji wao, Juma Banguke kupachika bao nne pekee yake katika mchezo wa mwisho wa hatua ya nane bora mtoani uwanja wa Kilakala Makaburini. 

Chenjela alisema kuwa mshambuliaji huyo alifanikiwa kufunga mabao mawili kila kipindi na kuiwezesha Mzinga kusonga mbele huku Saabasaba ikiondolewa katika mashindano hayo. 

Katika uwanja wa Shujaa timu ya Gereji yenyewe ilifanikiwa kuilaza Kihonda kwa kuitandika bao 1-0 huku bao pekee likipachikwa wavuni na mshambuliaji Nicolaus Kabipe katika dakika ya nane baada ya kuvunja mtego wa kuotea na kumchambua mlinda mlango wa Kihonda kufunga bao hilo kirahisi. 

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo mwamuzi wa kati, Simba Juma alijikuta katika wakati mgumu kufafanua sheria ya kuoktoe kufuatia mashabiki na wachezaji wa kata ya Kihonda  kuihujumu timu kwa kukubali bao linalodaiwa mfungaji, Nicolaus Kabipe alifunga bao hilo akiwa tayari ameotea na kudai mshika kibendera kushindwa kuona kosa hilo lililozaa bao katika mchezo huo. 

Akizungumzia ratiba ya mashindano hayo, Chenjela alisema kuwa michezo ya ligi ndogo ya kusaka mshindi wa kwanza, pili na tatu itaanza kutimua vumbi jumatatu kwa mchezo wa kata ya Boma kuanza karata yao dhidi ya Mwembesongo katika mchezo wa Shujaa wakati jumanne itachuana na Gereji na Mzinga.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: