Mshambuliaji wa timu ya soka ya wakuu wilaya nchini, Venance Mwamoto kulia akiwania mpira dhidi ya Willson Nkambaku kushoto wakati wa mazoezi ya kuajiandaa na mchezo wao na wabunge wa kukusanya fedha za ujenzi wa kituo cha maalbino kinachotarajiwa kujeng
wa Arusha juni 29 mwaka uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ambapo mazoezi hayo yanafanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.
PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Na Juma Mtanda,
Morogoro.
KATIBU wa michezo wa
timu ya netiboli ya wakuu wa wilaya wanawake nchini, Beatrice Mkassa amewataka
wapinzani wao timu ya wanawake wabunge wajiepushe kuchezesha mamluki katika
mchezo wao wa uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kituo cha ujenzi wa walemavu wa
ngozi (Albino) katika mchezo unaotarajia kufanya juni 29 mwaka huu katika
uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
mwandishi wa gazeti hili mjini Morogoro, Mkwasa alisema kuwa endapo timu ya
wabunge wanawake hatawaingiza mamluki katika mchezo wao dhidi ya wakuu wa
wilaya wanawake wategemee kuondoka na idadi kubwa ya vikapu vingi.
Mkwasa ambaye ni
nahodha wa timu hiyo alisema jeuri hiyo inatokana na mazoezi makali wanayofanya
na wachezaji wazuri waliowahi kutamba na timu mbalimbali waliowahi kutamba
kabla ya kuingia katika nyasfa hizo.
Timu yao iko imara
kila idara tofauti na timu ya wapinzani wao ambao katika michezo iliyopita
imekuwa ikichezesha mamluki na kamwe hawawezi kukwepa kichapo kwani kwa sasa
wana stamina ya kutosha ya kuwafanya kuwafunga idadi kubwa ya vikapu na kudai
kuwa timu hiyo sio mzuri ikilinganishwa na timu yao.
“Nawataka wapinzani
wetu timu ya wabunge wanawake wasiingie mamluki kwani lengo letu ni kuwafunga
idadi kubwa ya vikapu ili wakasimulie vizuri, nimewaona katika michezo yao
mingi ikiingiza mamluki na wakifanya hivyo watapunguza idadi ya vikapu” alisema
Mkwasa.
Mkwasa alisema kuwa
timu yao ina wachezaji wazuri wanaotosha kupata ushindi mnono mbele yao akiwemu
Sarah Dumba aliyewahi kutamba na timu ya redio Tanzania miaka ya 1980-1987
anayecheza nafasi ya ulinzi huku wengine kuwa ni Bituni Msangi anayemudu vema
nafasi ya ufungaji, Josephine Maturo nafasi ya golikipa wakati ikimtegemea
kiungo mchezeshaji, Mboni Mgaza.
Alisema kuwa kwa
wachezaji hao akiwemo na yeye mwenyewe atakayekuwa na kazi ya kumzuia kiungo wao
mshambuliaji atahakikisha hapati nafasi ya kugawa mipira ya mwisho kwa mfungaji
wao.
Mkwasa alisema kuwa
licha ya kupata mazoezi makali ya kuwakabili wabunge hao wanawake wamekuwa
wakifunza sheria mpya za mchezo chini ya Kocha wa Polisi Morogoro Edson
Chatanda ili wachezaji wake kujiepusha na madhambi yasiyo na lazima dhidi ya
wachezaji wa wabunge.
Kambi ya timu za
soka na netiboli imevunja kambi katika Manispaa ya Morogoro na kuelekea Dodoma
ambako watahudhuria kikao cha wakuu wa mikoa na wilaya ambako wakiwa huko
wanatacheza michezo ya kujipima nguvu dhidi ya timu tatu tofauti za CCM, CBI na
Tamisemi.
0 comments:
Post a Comment