Abubakar Adam (11) akiwa Hospitali ya Mount Meru mjini Arusha jana baada
ya kujeruhiwa wakati wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwenye mkutano
wa Chadema.
ARUSHA/DODOMA.
WAKATI watu waliofariki kwenye tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa Chadema ikifikia watatu baada ya jana kufariki kwa mtoto Amir Ally (7), mtoto mwingine wa miaka kumi na moja aliyejeruhiwa, amedai kwamba alipigwa risasi na polisi kwenye tukio hilo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye ametoa
tamko kuwa chama chake kina ushahidi wa kutosha wa watu waliohusika na
tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa kamp
eni wa chama hicho.
eni wa chama hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Arusha Medical
Lutheran Center (ALMC), Dk Paul Kisanga alisema jana kuwa, Amir
alifariki jana asubuhi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani
yaliyodhuru ubongo wake.
Dk Kisanga alisema huyo ni mmoja wa watoto watano,
waliojeruhiwa wakati wakitoka madrasa huko Kaloleni, jirani na Uwanja
wa Soweto kulipokuwa na mkutano na alifariki jana asubuhi hospitalini
hapo.
Alisema watoto wengine wawili ambao ni ndugu;
Fatuma na Sharifa Jumanne wamepelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi baada
ya miili yao kukutwa na vyuma.
Dk Kisanga aliwataja watoto wengine waliojeruhiwa kuwa ni Fahad Jamal (7) ambaye yupo ICU akisubiri timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kutoruhusu kusafirishwa.
Pia yupo Abubakar Adam (11) ambaye amejeruhiwa mguuni na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru.

Mtoto aeleza kupigwa risasi
Adam alisema jana kuwa alipigwa risasi na mtu
aliyekuwa amevalia sare za polisi, wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu
yake, Fahdi katika eneo la Soweto.
Alisema akiwa njiani, aliona watu wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa kupigwa risasi na kuanguka chini.
“Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa amevaa sare
za polisi,” alisema Adam mwanafunzi katika Shule ya Msingi Levolosi
huku akitokwa machozi.
Muuguzi wa zamu, katika katika wodi ya watoto
katika Hospitali ya Mount Meru, Asha Semdeli alisema jana kuwa mtoto
huyo ana vyuma viwili katika mguu wake.
“Tunasubiri afanyiwe upasuaji kwani tayari mashine
ya X-ray inaonyesha vyuma kuwepo katika mguu wa Adam siwezi kusema ni
risasi au la,” alisema Semdeli. CHANZO MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment