BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MZEE NELSON MANDELA AIFUNIKA ZIARA YA RAIS OBAMA BARANI LA AFRIKA.

http://www.channelnewsasia.com/image/715214/1371920410000/large16x9/768/432/barack-obama-listens.jpgRAIS Barack Obama anaanza ziara iliyosubiriwa kwa hamu barani Afrika, huku hali ya Nelson Mandela ikionekana kuiziba ziara hiyo, kwani macho na masikio yote yameelekezwa Afrika ya Kusini ambako Mandela yu mahututi. 

Familia ya Rais Obama inaondoka leo (26.06.2013) kwa ziara ya wiki moja barani Afrika itakayoifikisha nchini Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania kwa kile ambacho Ikulu ya Marekani inasema ni kuhamasisha demokrasia na fursa za kiuch
umi kwenye bara hilo lililo asili ya wazazi wa familia hiyo.

Lakini hali inayozidi kuzorota ya afya ya Mandela inaonekana kuitanda ziara ya Obama.

Shaka kwamba kiongozi huyo ambaye ni alama ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi duniani anaweza kuiaga dunia ndani ya siku chache zijazo, imezusha wasiwasi juu ya ratiba ya Rais Obama.

Tayari Ikulu ya Marekani imesema kwamba itashauriana na familia ya kiongozi huyo wa ukombozi nchini Afrika ya Kusini kuona ikiwa familia ya Obama inaweza kumtembelea hospitalini.

Mandela ni shujaa wa Obama
Mzee Nelson Mandela katika sherehe yake ya kuzaliwa miaka minne iliyopita. Mzee Nelson Mandela katika sherehe yake ya kuzaliwa miaka minne iliyopita.
 
Binafsi, Obama amewahi kumtaja Mandela mara kadhaa kama shujaa wake wa kisiasa, lakini tayari Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika ya Kusini, Maite Nkoane Mashebane, ameshasema kwamba ombi hilo halitawezekana kutekelezwa kwa kuwa Mandela yuko kwenye hali mbaya.

Mara ya mwisho Obama kuonana na Mandela ilikuwa ni mwaka 2005, pale Mandela alipokuwa mjini Washington, Marekani, na Obama akiwa ndio kwanza amechaguliwa kuwa seneta.

Hata hivyo, viongozi hao wawili wamewahi kuzungumza kwa njia ya simu mara kadhaa baada ya hapo, ingawa hapajawahi kuwapo kwa mazungumzo ya ana kwa ana kati ya maraisi hao wawili wa kwanza weusi kwa mataifa yao, tangu Obama kuingia madarakani mwaka 2008.

Ikulu ya Marekani inaichukulia ziara hii ya Obama kama nafasi ya kufidia muda mrefu ambao Rais Obama ameshindwa kupanga safari ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mara ya mwisho Obama kutembelea sehemu hiyo ya Afrika, ilikuwa ni pale aliposimama kwa muda nchini Ghana, mwaka 2009.

Fadhaa za Waafrika dhidi ya Obama
Wakati Nelson Mandela alipotoka jela mwaka 1990. Wakati Nelson Mandela alipotoka jela mwaka 1990.
Tangu mwanzo baadhi ya wachambuzi waliichukulia ziara hii ya Obama kama yenye lengo la kupunguza fadhaa za Waafrika kwa kiongozi huyo wa taifa kubwa duniani na mwenye asili ya bara hilo, lakini aliyeonekana kulipuuzia kwenye awamu ya kwanza ya uraisi wake.

Tayari ratiba ya Obama barani Afrika imeitenga Kenya na kuwakera wengi nchini humo, nchi ambayo ni nyumbani kwa baba mzazi wa Obama na ambako ndiko pia waliko ndugu zake wake wa ubabani.

Na sasa, ikiwa afya ya Mandela ndiyo itakayoamua jaala ya ziara ya Obama barani Afrika, na kwa hivyo kutokea uwezekano wa kushindwa kuzitembelea baadhi ya sehemu, kwa kushindwa kurefusha ratiba yake, hilo litaongeza fadhaa zaidi.
CHANZO  http://www.dw.de
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: