BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSHAMBULIAJI WA REAL MADRID, CRISTIANO RONALDO AFUMWA AKIFANYA MKUTANO WA SIRI NA VIONGOZI WA MANCHESTER UNITED.

cristiano ronaldo irina shayk basketball game 05
cristiano ronaldo hot pictures CRISTIANO Ronaldo bado hajamaliza hamu yake ya kujaribu kurejea katika klabu yake ya zamani ya Manchester United.

Taarifa zinaeleza kuwa atakutana na viongozi wa Manchester United ndani ya siku tatu zijazo na kujadili nao tena kama inawezekana kurejea au la.


Hata hivyo, tayari Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameishawahakikishia wanachama na mashabiki wake kwa mshambuliaji huyo mwenye tham

ani ya pauni milioni 80 ataendelea kubaki Bernabeu.

Gazeti la El Pais la Hispania limeeleza Mreno huyo atazungumza na viongozi hao wa Man United kabla ya kujiunga na Real Madrid kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Lakini kwa kuwa Fifa inakataza klabu kuzungumza na mchezaji yoyote mwenye mkataba unaozidi miezi sita, kila upande umeukana mkutano huo ambao gazeti hilo limesisitiza utafanyika.

Ronaldo alijiunga Real Madrid akitokea Man United ambako alijenga jina chini ya Kocha Alex Ferguson ambaye amestaafu baada ya kwisha kwa msimu uliopita.

Nyongeza:
Manchester United stats League - Apps: 196 Goals: 84
Cup - Apps: 38 Goals: 17
Europe - Apps: 55 Goals 16

Real Madrid stats League - Apps: 135 Goals 146
Cup - Apps: 20 Goals: 17
Europe - Apps: 40 Goals: 35
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: