Mhe Sugu
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda
BAADA ya kauli yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini dhidi ya Waziri
Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kufuatia majibu yake aliyoyatoa wiki iliyopita
Bungeni kwa kutaka Polisi kuendelea kuwapiga raia, Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe Joseph Mbilinyi 'Sugu', aomba radhi.
Sugu amemuomba radhi Mhe Pinda na watanzania kwa ujumla kwa lugha
aliyotumia katika kuonyesha hisia zake juu ya kauli aliyoitoa Mhe Pinda
bungeni.
Kupitia akaunti yake ya Facebook, Mbunge huyo machachari amenukuliwa
akiwaomba radhi Watanzania waliokerwa na kauli yake iliyodai kwamba
Tanzania haijawahi kuwapata Waziri Mkuu kama mpumbavu kama waziri mkuu Mhe. Pinda kwa kusema;
"Ndugu watanzania, naombeni radhi kwa tusi
nililolitoa kwa mhe Pinda, kwani nilikua nimeghafirika, halikuwa
kusudio langu kumtukana mmoja wa viongozi wa nchi."
0 comments:
Post a Comment