Sakata la kukamatwa makahaba hao lilijiri saa tisa usiku, Ijumaa
iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori jijini
Dar eneo ambalo makahaba wameligeuza ndio vyumba vyao vya biashara.
Kwa mujibu wa takwimu za kiserikali, eneo hilo (kuanzia Bamaga hadi
Sinza Mori) limekubuhu kwa wasichana kujiuza nyakati za usiku huku makao
yao makuu yakiwa eneo la Afrika Sana hasa pembezoni mwa Corner Bar.
“Tumejitahidi sana kushirikiana na polisi ili kutokomeza ukahaba eneo
hilo lakini wapi! Hawa mabinti ni wabishi, mbaya zaidi wamelifanya eneo
hili kuwa la ngono.
“Watoto wetu wanapita usiku pale wanawaona wanavyofanya, wanatuharibia
kizazi kijacho, kama wao wamejishindwa wasiwaambukize wengine.”
Siku ya tukio, saa tisa usiku, askari wa ulinzi shirikishi walijipanga
kwa ajili ya kuufumua mtaa huo huku wakiwa na tahadhari kufuatia habari
za kiintelijensia kudai kuwa, makahaba hao walipanga kuua mtu punde
watakapovamiwa.
Askari hao wakiwa kwenye doria ya kila usiku, waliwavamia makahaba hao
eneo lenye majani madogo katikati ya Afrika Sana na Mapambano upande wa
yadi ya Mwanamboka wakiwa na wateja wao wakifanya ngono hadharani.
Katika hali iliyoonesha makahaba wamejiimarisha kwa ulinzi siku hizi,
wakati wa zoezi hilo, machangu hao sanjari na vibaka wanaowaunga mkono
wakisemekana ni ‘walinzi’ wao, waliokota mawe na kuwarushia askari hao
hali iliyozua tafrani zaidi.
Ndipo piga nikupige ilipozuka ambapo askari walionesha umahiri wao wa
kupambana na wahalifu kwa kuwadhibiti kwa vichapo vya hapa na pale na
kufanikiwa kuwaweka wengi chini ya ulinzi.
Kuona hivyo, baadhi ya makahaba na wateja wao walifanikiwa kuwachoropoka
askari bila nguo na kutokomea gizani hivyo kulifanya eneo hilo kuwa
jeupe.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya makahaba waliokimbia
walijikuta wakiacha kwenye majani nguo zao za ndani na kuzua maswali
kwamba ni kwa nini hawakuwa wamezivaa!
“Jamani hizi si nguo zao za ndani ?.
Ina maana wakiwa kazini hawavai siyo? Wanakuwa tayaritayari kwa kazi? Jamani!” alisema kwa mshangao mkubwa mmoja wa askari hao.
Licha ya kuwa chini ya ulinzi mkali, baadhi ya makahaba walionaswa
walikuwa wakiwalalamikia askari hao kwamba wanawafuatafuata wakati kila
mtu siku hizi anaangalia atakulaje!
“Mnatuonea bure, nyie mnakula kivyenu na
sisi mngetuacha tule kivyetu, hao watoto wenu mnaosema tunawaharibu
usiku huu wao wanatokea wapi na wanakwenda wapi?” alisikika akisema kahaba mmoja aliyekuwa mtata kuwekwa chini ya ulinzi.
Mwingine akadakia: Kama mnataka tuwape
uroda si mseme, mnatukamata kila siku kwani tunawatibulia nini majumbani
mwenu? Lini tumekuja kuwaghasi wakati mmelala na wake zenu”
Uchunguzi wa kawaida ulibaini kuwa muda rasmi wa makahaba hao kuwasili
eneo la Corner Bar ili kuanza ‘kazi’ ni saa mbili usiku japokuwa wapo
wanaoripoti mapema na kufanya biashara hiyo kwa wizi kulingana na wateja
wenye ‘kiu’ nyakati hizo.
Licha ya kuwa chini ya ulinzi, makahaba hao waliahidi endapo watapelekwa
polisi na kutoka watarejea eneo hilo kujiuza kwani ndiyo ajira
inayowafanya waendelee kuishi katika Jiji la Dar es Salaam, kusomesha
watoto vijijini kwao na kuwasaidia wazazi wao mahitaji mbalimbali.
“Hata kama mtatupeleka polisi, tutarudi tu
hapa, sisi tunasomesha watoto, tunasaidia wazazi wetu vijijini, pia
tunaishi Dar kwa sababu ya kipato hiki cha kuuza miili yetu, acheni
hizo,” mmoja wa makahaba hao alisema bila kumung’unya maneno.
Akizungumza mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye pia ni askari wa ulinzi shirikishi alisema:
“Kufuatia vitendo hivi kushamiri hapa
mtaani hadi kufikia hatua ya makahaba na wateja wao kufanya ngono
hadharani kama wanyama, tuliamua kukimbilia polisi kutoa taarifa, kwa
hiyo tuna baraka za serikali za kuwatokomeza hawa machangu.”
0 comments:
Post a Comment