BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CPJ: TANZANIA LICHA YA KUWA NA SIFA NZURI LAINI INAWANYIMA WATU WAKE TAARIFA MUHIMU ZA HABARI.

Mwandishi wa Chanel Ten marehemu, Daud Mwangosi (mwenye kamera) akiwa mwenye furaha muda mfupi kabla ya kumkuta umauti akimchukua picha ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,  MICHAEL KAMUANDA kulia katika eneo la kijiji cha Nyololo mjini Iringa kabla ya kuanza kwa vurugu na hatimaye kufariki dunia hivi karibuni. ONGEZEKO la mashambulizi ya vyombo vya habari ni sehemu ya sheria kandamizi na udhibiti wa muda mrefu wa waandishi wa habari nchini Tanzania.
Kamati ya kulinda waandishi wa habari duniani katika ripoti yake iliyotolewa hivi karibuni Nairobi imesema licha ya sifa nzuri ya Tanzania iliyo nayo, watu wake wananyimwa taarifa muhimu.
Imeelezwa kuwa udhibiti wa muda mrefu wa gazeti moja la kukosoa unachangia hofu na udhibiti binafsi miongoni mwa waandishi wa habari nchini Tanzania.
Tom Rhodes mshauri na mwandishi wa ripoti wa CPJ Afrika Mashariki amesema mashambulizi ya hivi majuzi ya waandishi wa habari, pamoja na sheria zinazopinga vyombo vya habari, zinawafanya maripota kuhofia zaidi usalama wao.

"Udhibiti wa binafsi una maana ya kutoridhishwa kusikorekodiwa" amesema.

Ripoti, inayoitwa "Shida Isiyoonekana ya Vyombo vya Habari vya Tanzania," inataja mwiba katika mashambulizi na vitisho kama hivyo mwaka uliopita
-CPJ imeweka kumbukumbu 10 za miezi 11 iliyopita-ikiwa ni pamoja na polisi kumwua mwanakamera mkongwe alipokuwa akiangazia msafara wa upinzani lakini hakuna afisa yeyote aliyewajibishwa kwa mauaji hayo.

Ripoti hiyo pia inaulizia taswira ya kimataifa ya serikali ya Tanzania kuhusu kujitolea kwa uwazi na demokrasia, ikisema kuwa angalau sheria 17 zinazohusu ukandamizaji wa vyombo vya habari zingalipo.

Chini ya sheria hizi, gazeti moja la kukosoa, MwanaHalisi, limeondolewa kwa muda usiojulikana, hatua ambayo waandishi wengi wa habari wanaiona kama ujumbe unaotumwa kwenye mashirika yote ya vyombo vya habari.
 
Serikali imeahidi kurekebisha sheria za vyombo vya habari na imetia saini kwenye Mradi Huru wa Ushirikiano wa Serikali, juhudi za pamoja za kukuza uwazi. 
Ilhali baada ya miaka mingi ya majadiliano, haijatoa sheria ya kutekeleza ufikiaji wa taarifa au kubadilisha sheria mbalimbali zilizopo zenye vikwazo.
Mojawapo ya mapendekezo muhimu ya ripoti, CJP inasisitiza kuwa serikali inastahili kushauriana na vyombo vya habari na waandishi wa habari ili kutunga na kutekeleza sheria ya kufikia taarifa inayohakikisha kuwa wananchi wana ufikivu mpana wa nyaraka za umma.
Hata hivyo inastahili kuondoa vipengele na sheria zote zinazonyima uhuru wa vyombo vya habari na kuondoa marufuku na kuondoshwa kwa muda kwa vyombo vya habari.
Uchunguzi wa kina wa mashambulizi kwa waandishi wa habari lazima ufuatiliwe, ili wahusika washtakiwe kwa mujibu wa sheria. 
"Hatua za nidhamu za serikali ya Tanzania kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza ni ishara tosha kuwa inahisi kutishwa tunapokaribia uchaguzi wa urais na ubunge 2015," Rhodes alisema. 
 
"Lakini ili kutimiza viwango vya kimataifa vya uwazi na demokrasia, lazima serikali iwaruhusu waandishi wa habari kuripoti kuhusu kile kinachoendelea nchini bila hofu ya matokeo hasi" amesema.

Chanzo: CPJ
CPJ ni shirika huru, lisilo la faida linalofanya kazi ili kulinda uhuru wa vyombo vy habari duniani kote.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: