![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7stpfv8ITTPE10D7wZmIlORfjNGKSIV70h2bW3ZG1Ke9l8OquZKnn8Sk69bg0EVVU5BLNCDFGfEd93JtxO2zp06GXaGiP4-pKcStcf44zsN92MPedrHx-9jr4JhaYXUNIMJKNJVLyhSg/s640/CUFFF1.jpg)
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Uenezi wa Habari wa chama hicho, Abdul Kambaga, akiong
ea na NIPASHE jijini Dar es Salaam.
Alisema chama chake kimeaandaa vijana
watakaolinda amani kwa viongozi wao ili kuwaepusha na mabomu, wakati wa
mikutano na maandamano hayo.
“Serikali kwa kutumia polisi inawapiga wapinzani, CUF hawatuwezi, tutaandamana, tutafanya mikutano nchi nzima, alisema Kambaya.”
Katibu huyo wa Uenezi wa Habari,
alifafanua kuwa chama chao kimesajiliwa kisheria na kipo kwa mujibu wa
katiba ya nchi, hakioni sababu yakuzuiwa na polisi kila wanapotaka
kufanya mikutano yao kwa kisingizio kuwa Mtwara hakuna amani hata baada
ya tatizo la gesi kuisha.
Alisema kuwa chama chake kina vijana
waliosajiliwa kisheria kwa shughuli za chama kwa mujibu wa sheria ya
vyama vya siasa nchini, akadai kuwa CUF haioni sababu yakutofanya
maandamano na mikutano kwani bado viongozi wa chama hicho wanakamatwa,
wanapekuliwa na polisi bila sababu.
Hivi karibuni CUF kilizuiwa kufanya mikutano ikiwa ni pamoja na maandamano hasa mkoa wa Mtwara kutokana na tatizo la gesi.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
0 comments:
Post a Comment