SIMBA jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Kombaini ya
Polisi katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar
es Salaam.
Simba imepata sare hiyo baada ya kutoka kuchezea kichapo kutoka kwa
Coastal Union katika mechi nyingine ya kirafiki iliyochezwa mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Katika mechi hiyo, Simba ndio ilikuwa ya kwanza kuandika bao la
kuongoza katika dakika ya 15 kupitia kwa mshamb
uliaji wake mpya Betram
Mombeki.
Mombeki alifunga bao hilo baada ya kuwatoka mabeki wa Polisi ambapo
kwa kushirikiana vema na Sino Augustino aliachia shuti na kujaa wavuni.
Katika mechi hiyo, Simba ilicheza bila nyota wake wa kulipwa, hata mchezaji wake nyota Amri Kiemba jana pia hakucheza.
Polisi walisawazisha bao hilo katika dakika ya 57 kupitia kwa
Nicholaus Kabipe, bao hilo lilipatikana baada ya washambuliaji wa Polisi
kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Simba jana ilimchezesha Abdulhalim Humud, Jonas Mkude na Ramadhani
Chombo, kwenye kiungo wakati kwenye safu ya ushambuliaji iliwatumia
Mombeki, Agustino, Nasoro Masoud na Issa Rashid na kwenye nafasi ya
mlinda mlango alikaa Andrew Ntala ambaye hata hivyo alionekana kuwa na
mapungufu mengi kwani mipira ilimponyoka mara kwa mara.
Aidha Simba ilicheza vizuri katika kipindi cha kwanza, lakini hali
ilikuwa tofauti katika kipindi cha pili, hasa baada ya kuwatoa Hudud na
Chombo ambapo safu ya kiungo ilipwaya na ndipo Polisi walipotumia mwanya
huo kupata bao la kusawazisha.
Timu mbalimbali za Ligi Kuu zipo kwenye maandalizi, zikicheza mechi
za kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Agosti 24 mwaka huu.
Simba jana iliwakilishwa na: Andrew Ntalla, Nassor Masoud ‘Chollo’,
Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Miraj Adam, Rahim Juma, Jonas Mkude, Said
Ndemla, Abdulhalim Humud, Betram Mombeki, Sino Augustino na Ramadhan
Chombo ‘Redondo’.
Polisi FC: Kondo Salum, Eliasa Maftah, Simon Fanuel, Yahya Khatib,
Salmin Kiss, Salum Nahoda, Magige Machango, Andrew Bundala, Mokili
Lambo, Bantu Admin na Nicolas Kapibe.
Leo kwenye uwanja huo kutakuwa na mechi nyingine ya kirafiki ambapo
mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya
Turiani, Morogoro.
0 comments:
Post a Comment