MSHAMBULIAJI Didier Drogba ameendelea
kuwa mwiba kwa Arsenal akikumbushia enzi zake alipokuwa na jezi ya
Chelsea, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 leo kufunga
mabao mawili na kuiwezesha klabu yake, Galatasaray kutwaa Kombe la
Emirates.![Disappointment: Arsenal manager Arsene Wenger looks on during his side's defeat](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vZewvsYLxD9EjQU5KuML8Zbo9jHSTQ7pr57lAQEQdtkrOgkSQGwE0mSfvXMQNQVX1c9qtaQs4jTWkMIlRFL7tozDZ6GSHlV8fbIYJ-ys202ruzUW1PB67b3LVp7ZGH1XyACPnwhsuYQFejbsOkBAHWO5Y6IlG3Dtt_El0BOA=s0-d)
Kweli, ni mashindano ya kirafiki na
hayana maana yoyote katika msimu, lakini lilikuwa kama pigo lingine kwa
kikosi cha Arsene Wenger.
Mfaransa huyo aliwaka ile mbaya kana
kwamba mashindano hayo yana maana yoyote. Alimfokea refa wa akiba, Andre
Marriner baada ya refa Jon Moss kuwazawadia penalti wapinzani dakika 12
kabla ya filimbi ya mwisho kutokana na Ignasi’s Miquel kumsukuma
mshambuliaji huyo wa Ivory Coast.
Drogba alikwenda mwenyewe kupiga penalti hiyo na kumpeleka upande tofauti kipa Wojciech Szczesny na mpira alipoupiga.
Drogba akafunga tena zikiwa zimesalia dakika nne, baada ya kupokea pasi ya Wesley Sneijder na kumuacha Per Mertesacker, kabla ya kumtungua tena Szczesny.
Arsenal ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo dakika ya 38, mfungaji Theo Walcott.
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Gibbs/Miquel dk69, Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla/Zelalem dk61, Walcott na Sanogo/Giroud dk61.
Galatasaray Muslera; Semih, Riera, Chedjou, Eboue, Melo/Sarioglu dk66, Engin Baytar/Gulselam dk32,Altintop/Colak, dk45, Amrabat, Elmander/Drogba dk45, Umut Bulut/Sneijder dk45.
0 comments:
Post a Comment