MKE wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Mary
au Mama Gilo, mkazi wa Sinza jijini Dar amekula kichapo cha kutisha
almanusra apoteze uhai baada ya kunaswa akiiba nguo kwa ajili ya Sikukuu
ya Eid El Fitr.
Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na mwandishi wetu
lilijiri katika moja ya maduka makubwa ya nguo Kariakoo, Dar mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Mama Gilo ambaye anafahamika Kariakoo na Sinza, alinaswa akiiba nguo za sikukuu ikiwa ni pamoja na ‘madira’ ya kumalizia mfungo.
Katika
tukio hilo lililokusanya kadamnasi, mwanamke huyo alipigwa chabo kwenye
duka la mfanyabiashara Rehema Kessy ambapo alid
ai kuwa alifika Kariakoo
kwa lengo la kununua madira lakini alijikuta akiingiwa na tamaa ya
kuiba ndipo akanaswa.
Awali, kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi na raia
waliokuwa na hasira kali, mwanamke huyo alidaiwa kukwapua mkoba wa
mwanamke mwenzake na kujichomeka kwenye maduka kumkwepa aliyemuibia
‘pimajoto’ lake linalodaiwa kuwa na vitu ndani yake.
Baada ya kutiwa mikononi ndipo watu waliokusanyika wakauliza: “Na tumfanye nini mwanamke huyu?”
Watu
wakapaza sauti wakisema: “Kwa utaratibu wetu hapa Kariakoo kwa mwizi
yeyote, hakuna adhabu nyingine zaidi ya kusulubiwa hadharani.”
Ndipo
ikaamriwa asulubiwe kwa kupewa bonge la kipigo na kufanya watu kutanda
kwenye duka hilo kwa muda wa saa nzima bila kutoka, wakitaka aachiwe ili
wamalize kazi yao ya kumtoa roho kama adhabu ya mwizi anapokamatwa
Kariakoo.
Katika kusulubiwa huko, Mary alikuwa akilia kwa uchungu
mkubwa akisema: “Naombeni mnisamehe, nimekuwa nanyi siku zote tukifanya
biashara ya madira, leo mnaniua? Naombeni mumpigie simu mume wangu baba
Gilo aje anisaidie.”
Alipoambiwa
akiri kuhusika na upotevu wa madira madukani katika mazingira ya
kutatanisha kisha atasamehewa, alisema: “Ni kweli nakiri mbele yenu na
Mungu awe shahidi, nimekuwa nikifanya kazi hii (kuiba madira) pamoja na
wanawake wenzangu watatu lakini wamenikimbia.”
Kwa mujibu wa
mashuhuda wa tukio hilo, si mara ya kwanza kwa Mary kukamatwa kwa wizi
kwani mwanzo aliwahi kudakwa, akavuliwa mpaka nguo lakini amerudia tena
kazi hiyo.
Ili kumnusuru, mmoja wa wasamaria wema aliyehisi uchungu
kwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akilalamika kuwa anakata roho, aliwapigia
simu polisi wa Kituo cha Msimbazi, Kariakoo na kuwaambia: “Wahini mara
moja hapa jirani na shimoni. Kuna mwanamke mwenye hatia ya wizi
anasulubiwa. Njooni mumuokoe.”
Ndani ya ‘dakika sifuri’ polisi na
ulinzi shirikishi walifika eneo la tukio lakini walipomuona mtu
waliyekuja kumuokoa akiwa ameshalegezwa , ikabidi waagize tolori la
kumbebea.
Tolori liliposogezwa jirani na mwanamke huyo alipakizwa na
kumkimbiza huku wananchi wakimsindikiza kwa kumzomea wakati wengine
wakitaka kumponda na mawe hadi afe.
Mwisho wa yote mwanamke huyo
alikwenda kubwaga kituoni Msimbazi akiwa amepoteza fahamu kisha
kufanyiwa utaratibu wa matibabu kabla ya kesi .
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / KUELEKEA SIKUKUU YA NANE NANE NA EID EL FITR, MKE WA MTU ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUNASWA AKIIBA NGUO KARIAKOO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment