BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIZI NDIZO SABABU ZA WATOTO KUSHINDWA KUJUA KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU SHULENI.

NJE ya darasa la pili katika Shule ya Msingi Ilala iliyopo Manispaa ya Iringa, baadhi ya wanafunzi wanamsimanga mwenzao mmoja kwa kumwita mtoro.
 
Mmoja anapaza sauti na kusema:  “Sharafi hajui kusoma’’ Ni kweli Sharafi (jina siyo lake) anayesoma darasa la pili shuleni hapo, anaelezwa na mwalimu wake kuwa hajui kusoma na pia ni mtoro aliyekubuhu, japo mwenyewe anakana kuwa siku hizi siyo mtoro tena.

Mwalimu wake Esther Sanga, anasema  baadhi ya wanafunzi darasani mwake wana matatizo ya kutokujua kusoma licha ya kuwa hivi karibuni watamaliza darasa la pili, akiwamo Sharafi anayesema anaweza kukaa hata mwezi mmoja hajaonekana shuleni.

Tukiwa darasani namwomba mwalimu huyo tumjaribu Sharafi kujua uwezo wake wa kusoma.  Tunamwandikia ubaoni neno ‘baba’, kwa sekunde zisizozidi 10 analisoma na kulipatia. Kisha tunamwandikia neno ‘iba’, akachukua sekunde zaidi kulisoma na kulipatia.

Neno lingine lilikuwa ‘bobu’. Hapa Sharafi anatafakari zaidi huku akilikazia macho neno hilo.  Baada ya sekunde nyingi kupita anafanikiwa kulisoma kwa usahihi japo anaonyesha kutokujiamini na alichokisoma.
Darasa analosoma lina watoto karibu 40 ambao licha ya kubakiwa na muda mchache kujiunga na darasa la tatu, bado hawajaweza kusoma kwa ufasaha hasa herufi mwambatano,

Mwalimu Sanga anasema wanafunzi hao wanasoma, lakini kwa kile anachokiita usomaji wa kudonoadonoa. Anasema: ‘’ Hawa wanasoma kwa kudonoadonoa, hawasomi kwa mfululizo na sababu ni kwamba wako wengi darasani na walikosa walimu wenye ujuzi.’’

Bila shaka wanafunzi hawa ni ushahidi wa kuwapo wanafunzi wengi wanaovuka darasa la pili wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, maarufu kwa kifupi cha KKK au K3 Ilivyo mfumo wa elimu wa Tanzania, unamtarajia mtoto akimaliza darasa la pili awe ana uelewa mkubwa wa stadi hizo -muhimu katika mchakato wa ujifunzaji.

Kisa cha Shule ya Msingi Ilala kinashadadiwa na matokeo ya utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Uwezo Tanzania, na kubaini mwanafunzi mmoja kati ya watano wanaohitimu elimu ya msingi, hajui kusoma japo hadithi ya kiwango cha darasa la pili.

Utafiti huo  ulioitwa ‘ Je watoto wetu wanajifunza? Ulihusisha sampuli ya  watoto 42,033 kutoka kaya 22,800 katika wilaya mbalimbali nchini. Watoto hao walipimwa uwezo wa kusoma na kuhesabu. Sababu za kutojua kusoma. MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: