BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MATAPELI YAWATOKEA PUANI UTAPELI, WAONJA ADHA YA KIPIGO BAADA YA ZOEZI LA KUTAPELI KUSTUKIWA NA WANANCHI, MWANAMKE AWAPONZA JIJINI DAR ES SALAAM.




Wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakiwahoji matapeli ambao walikua wakijaribu kumfanyia utapeli dada mmoja na hatimaye kushindwa kutimiza lengo lao mara baada ya dada huyo kushtukia mbinu zao na kuomba msaada kwa wananchi na ndipo hapo walipotiwa nguvuni na kupelekwa katika ofisi za serikali ya mtaa wa migombani Matapeli (mwenye shati la draft) wakipewa kichapo mara baada ya kushindwa kujibu maswali ya wananchi waliowakamata leo katika kituo cha daladala cha Segerea

Mmoja wa watumishi wa serikali ya Mtaa wa Migombani Kata ya segerea Mfaume (wa kwanza kushoto Mwenye fulana ya njano) akijaribu kuwakata wananchi hao kujichukulia sheria Mikononi mara baada ya kuwatia nguvuni matapeli hao leo katika kituo cha daladala cha Tabata Segerea

Mmoja wa matapeli akijizuia kichwani mara baada ya wananchi wenye hasira kali wakiendelea kushusha kipigo kitakatifu, katika tukio la kujaribu utapeli lililotokea muda mfupi katika kituo cha daladala cha segerea mwisho

Hapa tapeli wa pili (aliyeinamishwa kichwa) akiendelea kupokea maumivu kutoka kwa wakazi wa segerea mara baada ya kukamatwa wakati wakitaka kujaribu kutapeli



kipigo kikiendelea kutolewa kwa matapeli hao


Matapeli wakiwa ndani ya ofisi ya serikali ya mtaa wa migombani mara baada ya kupokea kipigo cha mbwa mwizi muda mfupi uliopita katika kituo cha daladala cha segerea mwisho wakati wakijaribu kutapeli

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakichungulia dirishani katika ofisi za serikali ya mtaa wa migombani kwaajili ya kushuhudia matapeli waliopokea kichapo cha mbwa mwizi mara baada ya mbinu zao kufua dafu na kushtukiwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: