BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LUNYAMILA AONDOLEWA MASHINE ZA OXYGEN, HALI YAKE YAIMARIKA.


LUNYAMILA.


HALI ya winga nyota wa zamani wa Yanga na Simba, Edibily Lunyamila imeimarika kwa jioni hii.





Lunyamila amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.


Taarifa zilizotufikia punde, Lunyamila anaendelea vizuri ukilinganisha na mchana.


Mashine za msaada wa kupumua zimeondolewa na sasa anaweza kupumua mwenyewe.

Ndugu yake wa karibu amesema kuna nafuu ingawa bado hali yake haijaiamarika sana.
“Bado haijawa nzuri sana lakini sasa ni afadhari,” alisema. 



Lunyamila ambaye sasa ni mchambuzi wa masuala ya soka katika gazeti la CHAMPIONI ameanza kusumbuliwa na presha hivi karibuni. 



Mwanasoka huyo aliyechipukia kisoka mkoani Shinyanga ingawa ni mwenyeji wa Kigoma alikuwa akisifika kwa kasi na mashuti makali wakati anakimbia na mpira lakini krosi za maana.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: