Ndege hiyo ilikuwa ikielekea London Uingeleza jana na baada ya kupata ajali hiyo abiria wote walishushwa salama na kupelekwa hotelini,mpaka sasa inasemekana ndege hii imeingia dosari japo bado haijathibitishwa vizuri.
Mwanahabari Harriet Tolputt ali-tweet tuhuma kuhusu ajali hiyo baada ya abiria wa daraja la kwanza kuanza kushushwa kwanza na kisha abria wa madaraja mengine kusubiri kitu ambacho hakikua kizuri hasa kwa wakati wa dharura kama ile.
Harriet Tolputt aliandika ‘Abiria yeyote ambaye yupo karibu na mlango wa dharura anaweza kutoka bila kujali daraja lake kwa sababu ni muda wa hatari ndege ikiwa imegonga sehemu kama ile’.
Chanzo kikuu cha ajali hiyo bado kipo kwenye uchunguzi chini ya South African Civil Aviation Authority (SACAA)
0 comments:
Post a Comment