MWANDISHI na Mtangazaji wa kituo cha luninga cha SUA Morogoro Kelven Gwabara kulia akiwawishiwa kununua miti ya mkrismas kwa ajili ya mapambo hasa katika sikukuu ya krismas inayosherehekewa duniani kote na waumini wa dini ya kikristo, hapa ni mtaa wa Luna barabara ya Madaraka mji Morogoro.PICHA/MTNADA BLOG
HUYU katikati ni mtawa wa kanisa katoliki akiwa amezungukwa na wafanyabiashara wa kuuza maua wakati naye akiwawishiwa kununua kwa ajili ya mapamba ikiwa ni maandalizi ya sikukuu hiyo.PICHA/MTNADA BLOG
HEKAHEKA iliendelea kama kijana huku akionekana akiwa na baiskeli iliyobeba mti wa mkrismas wakati akisaka wateja wa kuwauzi katika barabara ya old Dar es Salaam.PICHA/MTNADA BLOG
MWENDESHA bodaboda naye akiwa amepewa kazi ya kubeba miti hiyo wakati akipeleka mtaa wa Luna kwa ajili ya mauzo.PICHA/MTNADA BLOG
HII ilikuwa ajali barabara ya BOMA ambayo ipo katika kata ya Mhe Amir Juma Nondo ambaye ndiye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro baada ya kugongana na pikipiki nyingine katika eneo la kona kabla ya kuingia mashamba ya wafungwa ukielekea katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Morogoro hivyo iwe kwa mtembea kwa miguu, mwenyesha chombo cha moto kuchukua tahafadhali kwani siku kama ya leo wengi wamekuwa wakitumia vyombo hivyo pasipo uangaliafu wa kutosha kutokana na baadhi ya kuonywa vinywaji vinavyoivuruga akili yao.PICHA/MTNADA BLOG
HUYU ni Juma Mtanda ambaye ni mmiliki wa blog Mtanda Blog akifanya mazoezi ya kuogelea katika bwawa la kuogelea la Nashera, watalaam wa mazoezi wamebeinisha kuwa mazoezi ya kuogelea ni mazoezi mazuri kuliko mazoezi yote kutokana na sababu kila kiungo kufanya kazi wakati ukipiga mbizi.PICHA/MTNADA BLOG
WATOTO nao hupenda mchezo wa kuogelea kama wanavyoonekana watoto hawa wakimlazimisha mwenzao aingie katika maji jambo hili sio zuri kwani kunaweza kutokea hatari hivyo wazazi wanaoongoza na watoto kwa manajili ya kuwapeleka kuogelewa wanapaswa kuwa karibu nao na kukemea hatari zinazofanywa na watoto hao ili kuepuka kuumia na pengine kunywa maji. PICHA/MTNADA BLOG
0 comments:
Post a Comment