FAHAMU HAYA KUHUSU MENO YA TEMBO NA BIASHARA YAKE
Yafuatayo kuhusu biashara ya meno ya tembo
Kwanza: Matumizi yake; meno ya tembo hutumika kutengeneza vitu vya urembo kama vile hereni , mikufu, mapambo kama vile sanamu na hata keys za keyboards za vinanda.
Vifaa vilivyotengenezwa kwa meno ya tembo hutumika nchini China kama sehemu ya kuonyesha ufahari, kwa mujibu wa Wikipedia.
Pili: Bei ya meno ya tembo
Bei inategemea na soko , hata hivyo kwa mujibu wa answers.com , jino moja la tembo huweza kuuzwa kwa dola za kimarekani mia saba (700).
Elewa jino moja la tembo linaweza kuwa na kilo zisizopungua arobaini (40) kwa tembo wa bara la Asia wakati Africa hufikia hadi kilo 90 kwa mujibu wa ANSWERS.COM. Tembo wa kiume na waliokua tayari ndio haswa husakwa.
TEMBO ALIYEUAWA NA KUTOLEWA SEHEMU NYAMA INAYOSHIKILIA PEMBE ZAKE BAADA YA KUUAWA.
Tatu: Wapi wananunua meno ya tembo ?
Kwa mujibu wa dailymaily.co.uk , vinara wa ununuzi wa meno ya tembo. China ndio namba moja duniani ikifuatiwa na namba mbili Marekani. Zipo nchi nyingine duniani ambapo meno ya tembo hutumika kutengeneza vifaa hivyo
Nne: Wanyama wengine wanaotafutwa: Meno ya kiboko pia hutumika kutengeneza vifaa kama hivyo vilivyotajwa ambavyo vinatengenezwa kwa meno ya tembo.
0 comments:
Post a Comment