
Aidha mashabiki na wadau wa muziki wa dansi walionyesa kukunwa na ubora wa sauti za waimbaji wa bendi hiyo wakiongozwa na Choki, Banza Stone,Athanas Muntanabe na Richard Maarifa na Adam Bombole.Safu ya unenguaji ya bendi hiyo ikiongozwa na Super Nyamwela,
Otilia Boniface alilishambulia jukwaa kwa shoo mpya ya Kimbembe na kuwafanya mashabiki wengi walihudhuria onyresho hilo kushindwa kutulia vitini hali iliyoleta msisimko mkubwa ukumbini hapo.
Katika onyesho hilo Extra ilisindikizwa na bendi ya Mashujaa ambayo nayoilifanya mambo sawasawa, huku pia malkia wa mipasho Khadija Kopa akinogesha uzinduzi huo.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Lina Sanga na Amin nao walikuwa sehemu ya burudani muhimu zilizopamba ukumbini hapo na kufanya onyesho kuacha midomo wazi wadau wa muziki waliofurika ukumbini hapo.
Siku chache kabla ya uzinduzi huo,Uongozi wa wakali hao wa muziki wa dansi nchini Extra Bongo Next Level Wazee wa Kimbembe ulimrejesha kundini aliyewahi kuwa rapa bendi hiyo Greyson Semsekwa sambammba na kumnyakuwa mnenguaji Asha Sharapova kutoka bendi ya African Stars Twanga Pepeta.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, alisema, kurejea kwa Semsekwa mmoja ya wanamuziki waasisi wa Extra Bongo kumezidi kuimarisha safu ya 'kufokafoka' wakati wa uzinduzi wa albamu yao mpya ya 'Mtenda Akitendewa' inayoendelea kuzinduliwa katika kumbi mbalimbali za starehe ndani na nje ya nchi.
Semsekwa alishiriki kwa kiwango kikubwa katika albamu ya 'Mjini Mipango' mwaka 2009 kabla ya kutimkia Twanga Pepeta na sasa amerejea kundini akiwa na rapu mpya ambazo anaendelea kuztaimbulisha katikaa maonyesho maalumu ya Utambulisho wao litakalofanyika katika Ukumbi wa Meeda Sinza.
comAlisema, wameamua kumchukua Sharapova baada ya kutambua kipaji alichonacho katika unenguaji hivyo kukidhi vigezo vya kunengua kwenye bendi hiyo inayoundwa na wanenguaji wakongwe kama Maria Salome na Otilia Boniface chini ya ukufunzi wa Super Nyamwela.
"Tunaendelea na mikakati ya kujiimarisha kwakuwa kila maboresho tunayofanya kwenye bendi pia tunazingatia maoni na ushauri wa wapenzi na wadau wa Extra Bongo ili kuendelea kuwapa burudani inayowasuuza nyoyo zao,"alisema Kasesa. Aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika maonyesho mbalimbali ya bendi hiyo kuona muonekano mpya wa Semsekwa na Sharapova baada ya kutoka Twanga Pepeta. http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment