KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempitisha
Grace Tendeya Mvanda, kuwa mgombea wake katika kinyang’anyiro cha ubunge
katika jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.
Grace Mvanda alikuwa
mtu wa pili katika kinyang’anyiro cha kura za maoni jimboni humo.
Aliyeshika nafasi ya kwanza alikuwa ni Lucas Sinkala Mwenda (31) ambaye
Kamati Kuu haikupitisha jina lake.
Mwenda ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sheria na sasa anataka kujiunga na Mafunzo ya Sheria kwa vitendo.
Uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga umepangwa kufanyika 16 Machi 2014.
Uchaguzi huu unatokana na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk. William
Mgimwa kufariki dunia miezi miwili iliyopita nchini Afrika Kusini.
Taarifa za ndani ya kikao zinasema, Kamati Kuu ilijadili kwa kina
majina ya wagombea wote wa nafasi hiyo; huku wajumbe wakipata nafasi ya
kuwahoji kila mgombea aliyekuwa anatafuta nafasi ya kupeperusha bendera
ya chama.
Hatimaye Grace Masha, kwa kutumia ripoti za
interejensia ya chama na vigezo vingine, aliteuliwa kuwakilisha chama
katika kinyang’anyiro hicho.
Miongoni mwa vigezo vilivyotumika,
ni kwamba mwanamama huyo aliwahi kugombea ubunge katika jimbo hilo
mwaka 2005 kupitia chama cha Jahazi Asilia. Alishindwa.
Lakini
alishika nafasi ya pili nyuma ya mgombea wa CCM. Taarifa zinasema,
pamoja na kwamba JAHAZI Asilia hakikuwapo jimboni humo na mkoa wa Iringa
kwa ujumla, lakini alifanikiwa kujinyakulia kura 13.500.
“Hii inaonyesha mgombea huyo anakubalika,” anaeleza Tundu Lissu, Mwanasheria mkuu wa chama hicho.
Lucas Sinkala Mwenda, alikubaliana kwa moyo mmoja na maamuzi ya Kamati
na ameahidi kutoa ushirikiano kwa mgombea na kukisaidia chama chake
kushinda.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / CHADEMA LAPITISHA JINA LA GRACE MVANDA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALANGA IRINGA,
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment