BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHADEMA YAPATA PIGO.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_jurVQSTWf4EbcTwLj0xdjjDUvHIYa5p622NtV7KaxWH55eq6U9lmMmKQ00XDFbN3uSwZGHOFUxp0OtC5EQXTOAg3qofAwlAwBHOs2tNgaQ5or4Kc-aFhFxVWAvZDqPfoimWEJtR9uTc/s1600/SLAA.JPG KATIBU MKUU WA CHADEMA DK SLAA.

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Shinaynga kimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wawili katika manispaa ya Shinyanga kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na madai kuwa viongozi ngazi ya taifa wa chama hicho kundekeza majungu,migogoro ,kudhalilisha baadhi ya viongozi pamoja na kuwapa majina ya wasaliti wa chama. 



Madiwani waliofikia maamuzi hayo magumu ni diwani wa Kata ya Ngokolo Sebastian Peter maarufu OBAMA WA NGOKOLO na Zacharia Mfuko wa kata ya Masekelo ambao wamesema wameamua kufikia maamuzi hayo magumu kama ishara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho kitaifa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: