
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiweka shada la maua katika Makumbusho ya Mahatma Ghandhi Mjini New Delhi, ambayo ni sehemu maalum iliyotayarishwa kwa wageni mbalimbali wanaofika katika Makumbusho hayo, Rais akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake nchini India.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Tanzania nchini India John W.H.Kijazi walipofika katika Makumbusho ya Mahatma Ghandhi Mjini New Delhi India na kuweka shada la maua katika makumbusho hayo, akifuatana na ujumbe wake katika ziara ya siku tatu nchini humo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na ujumbe wake wakielekea katika sehemu maalum iliyotengwa kwa shuhuli ya uwekaji wa maua kwa wageni mbali mbali wanaofika sehemu hiyo ya Makumbusho ya Mahatma Ghandhi mjini New Delhi India.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na mwenyeji wake MakamU wa Rais wa India Mohammed Hamid Ansari, mara alipowasili Ofisini kwake Mjini New Delhi,akiwa na ujumbe aliofuatana nao wakiwemo Mwaziri mbali mbali na makatibu. (Picha na Ramadhan Othman, India)
0 comments:
Post a Comment