BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FFU YAFANYA KAZI YA ZIADA IKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA WAKULIMA MELELA KATIKA BARABARA KUU IRNGA- MOROGORO


Askari wa Kikosi cha kutuliza Fujo Akizima Moto uliowashwa na wakulima waliofunga barabara ya Morogoro Iringa Leo Asubuhi.Wakulima hao walifunga Barabara hiyo kwa Lengo la kushinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Joel Bendera Ili kutatua Mgogoro uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopo katika vijiji hivyo.Askari wa jeshi la Polisi walilazimika Kutumia Mabomu ya Machozi mara baada ya Wananchi wao kugoma Kuonana na Kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mvomero Ikiongozwa na Mkuu Wa Wilaya ya mvomero

Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wamishika mawe na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiyo wakitaka Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.


Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji. Wakulima wa kijiji cha Mangae wilaya Mvomero wamefunga barbara kuu ya Morogoro Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba yaliopo eneo la Mkangazi
baada ya wananchi kuvamiwa na kupigwa wakulima hao walikusanyikajana usiku na kufikia maamuziWakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha mgongamano mkubwa wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa. Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo
Askari wa Jeshi la Polisi Wakiwa Onyo wakulima wa Kijiji Hicho Kabla ya Kuanza Kutumia Mabomu ya Kutoa Machozi kwa Lengo la Kuwatanya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: