BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JUMBA LA MAKUMBUSHO LA KIMATAIFA LIPO KATIKA HATARINI YA KUSHAMBULIWA NA KUNDI LA KIGAIDI LA AL-SHABAB NCHINI UGANDA.

Wapiganaji wa Al-Shabab.

UBALOZI wa Marekani Kampala wasema kuna ishara kwamba jumba la makumbusho la kitaifa ni mojawapo ya majengo yanayolengwa na magaidi

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umeonya juu ya uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Kampala.


Katika ujumbe uliotolewa Jumatatu jioni, ubalozi huo ulisema umepata habari kwamba huenda kundi la washambuliaji likiwa tayari kuvamia malengo kadhaa mjini Kampala mwezi Februari na Machi.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa kuna ishara kwamba jumba la makumbusho la kitaifa ni mojawapo ya majengo yanayolengwa. Lakini serikali ya Uganda haijatoa tamko la haraka juu ya onyo hilo.

Ujumbe huo haujawaonya Wamarekani kuondoka Kampala lakini umewatahadharisha kuepuka jumba la makumbusho na maeneo mengine yenye watu wengi.


Kundi la al-Shabab kutoka Somalia lilifanya shambulizi la kigaidi huko Kampala Julai 2010 na kuuwa watu 70.  http://www.voaswahili.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: