Leo Polisi Moro SC imerejea ligi kuu ya vodacom Tanzania bara baada ya kuilaza MajiMaji ya Songea katika mfululizo wa michezo ya ligi daraja la kwanza Tanzania kwa msimu wa mwaka 2013/2014 ambapo katika mchezo huo MajiMaji ilikukubali kipigo cha bao 2-1 kilichowapa nafasi Polisi Moro SC kukusanya pointi 25 na kutangaza kupanda ligi kuu huku katika kundi hilo ikiwa imebakiwa na michezo miwili ya kuhitimisha mzunguko wa pili. PICHA/MTANDA BLOG.
Timu ya JKT Mlale yenye pointi 17 ndiyo ilikuwa ikiifukuza Polisi Moro kwa kushika nafasi ya pili na kuifanya timu hiyo ya maafande hata kama itashinda michezo yake miwili iliyobakia kufikisga pointi 23 ambazo tayari Polisi Moro imezivuka.
JKT Mlale nao leo ilikukubali kupigo kutoka kwa Lipuli ya Iringa kwa bao 2-0 mchezo uliofanyika Mjini Songea na kuicha Polisi Moro isiwe na presha yoyote ya kuendelea kushika ushukani wa kundi lao.
0 comments:
Post a Comment