Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa nyuma kwa
tofauti ya pointi nne kwa Azam (43) na mchezo moja mkononi kulinganisha
na vinara hao ambao hawajapoteza mchezo wowote hadi sasa.
Mdachi huyo aliliambia gazeti hili kuwa wachezaji
wake wanapaswa kuuchukulia umuhimu mkubwa mchezo huo kwani ndiyo
utakaotoa mwelekeo wao wa kutetea ubingwa wao msimu huu.
Pluijm alisema Azam ni timu ngumu na haijapoteza
mchezo wowote tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi hivyo kama wakishindwa
kuwafunga basi wanaweza kujikuta katika hali mbaya zaidi.
“Maandalizi yetu yanakwenda vizuri. Nashukuru
wachezaji wangu wako vizuri isipokuwa Mrisho Ngasa ambaye bado anaumwa,
lakini wengine natumaini wataziba nafasi yake.
“Nauchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa,
hatupaswi kupoteza mechi hii kwani matokeo yoyote mabaya tutakayopata
yatatuweka katika mazingira mabaya. Ukiangalia Azam ndiyo wapinzani
wetu wakubwa sasa, hivyo hatuna budi kujitahidi na kuhakikisha
tunawafunga.
Pia, Pluijm amewalalamikia washambuliaji wake kwa
kukosa umakini wanapolifikia lango la wapinzani kwani ilichangia kukosa
ushindi Jumamosi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kocha huyo anaamini kama washambuliaji wake
Emmanuel Okwi, Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wangekuwa makini basi
wangeibuka na ushindi mnono.
“Tulicheza vizuri na tulistahili kushinda mchezo
ule, lakini washambuliaji wangu walikosa magoli mengi kwa sababu
hawatulii. Wanapolifikia lango, wanatakiwa kubadilika na kuona kuwa
tunausaka ubingwa kwa hali yoyote.
“Muda umeisha na zimebaki mechi chache kabla ya
msimu kumalizika. Wachezaji wote wanatakiwa kutambua hilo na kutimiza
ipasavyo majukumu yao uwanjani ili tuweza kutetea ubingwa wetu,”
alisisitiza Pluijm.
0 comments:
Post a Comment