HII NDIYO RIPOTI YA WATOTO WA TANZANIA AMBAO WAMELAWITIWA KIPINDI CHA MWAKA 2013.
Ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania imesema watoto wapatao 800 walilawitiwa mwaka 2013.
Ripoti ya shirika hilo inasema kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto nchini Tanzania ambapo kumi kati yao wakiwa wamefanyiwa ukatili huo na wazazi wao wenyewe.
Akiongea na BBC mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Dr Helen Kijo-Bisimba amesema watoto wamekuwa katika maisha ya hatari zaidi nchini humo kutokana na watu wa karibu wakiwemo wazazi wa kiume na hata kaka na wajomba zao kubainika wanawafanyia vitendo vya ubakaji.
Pia utafiti huo umeonyesha kuwa watu zaidi ya 1600 wakiwemo askari polisi wanane, waliuawa na wananchi wenye hasira kali katika matukio tofauti huku askari polisi nao waliwaua raia 28 katika kipindi cha mwaka 2013. BBC
0 comments:
Post a Comment