WATU zaidi ya 10 wametapeliwa fedha, walizotuma kwa mtandao baada ya kurubuniwa kuwa wangepata mikopo katika taasisi, iliyojitambulisha kwa jina la Savings Foundation Loans na kudai ofisi zake ziko katika Jengo la Utumishi. Wanadaiwa kutoa kati ya Sh 50,000 na 100,000 kwa watu hao, wanaodaiwa ni matapeli, wakitumia jina la Menejimenti ya Utumishi wa Umma Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Florence Temba alimwambia mwandishi watu waliotapeliwa, wamekuwa wakifika ofisini hapo kufuatilia mikopo hiyo.
Kwa mujibu wa Temba, miongoni mwa waliotapeliwa, wamo wakazi wa mikoa mbalimbali nchini, ambao wamekuwa wakipiga simu, kuulizia mikopo hiyo baada ya kutakiwa na watu hao kutoa fedha.
Taasisi hiyo ya kitapeli, ilielekeza watu kuwa makao makuu yake yako Dar es Salaam, Jengo Kuu la Utumishi wa Umma “Ofisi ya Rais” kitengo cha Mikopo na Uwekezaji, Jengo Namba 360, ghorofa namba moja Customer Service fund.
Temba ambaye ofisi yake jana ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari, kuonya wananchi juu ya utapeli huo, alisema hiyo ni mara ya pili kuhadharisha, lakini wamekuwa wakipokea maswali kutoka kwa wananchi huku taasisi hiyo ikiendelea kuwatapeli kwa kutoa namba zaidi kwa ajili ya kutuma fedha.
Wakati huo huo, polisi imesema utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti, umeenea nchini na kutaka wananchi kuuliza kabla ya kuamua kufanya jambo lolote.
Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso aliliambia gazeti hili jana Dar es Salaam kwamba matapeli hao, wamekuwa wakitangaza vitu ambavyo havipo kiuhalisia na kuwafanya wananchi kuingia katika mkumbo.
Senso alisema hayo kutokana na hadhari ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa wananchi dhidi ya utapeli, unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti.
TCRA imetaka wanajamii kutokutoa simu wala kadi ya simu kwa mtu asiyefahamika, kuitumia. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, mmiliki yoyote wa simu, asitoe maelezo yoyote kuhusu namba ya simu au taarifa za binafsi kwa mtu atakayempigia kutaka taarifa.HABARILEO
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MAPETELI WA MIKOPO WATAPELI WATU 10 HUANZA NA KIASI CHA SH50,000 HADI SH100,000 JIJINI DAR ES SALAAM.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment