RONALDO PONTILLAS.
Na Asha Said.
BONDIA Ronald Pontillas, atawasili nchini kesho asubuhi kwa ajili ya pambano lake la kimataifa dhidi ya bondia Francis Miyeyusho, litakalofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es
Salaam jana, mratibu wa pambano hilo Mussa Kova, alisema kuwa Pontillas raia wa
Ufilipino, atawasili nchini akiwa na kocha wake, Amogo Samson.
Kova alisema bondia
huyo atawasili majira ya saa moja asubuhi,
akitumia ndege ya
Qatar Airways.
Alisema kuwa moja kwa
moja ataenda hotelini kupomzika kabla
ya saa 5, kuzungumza
na vyombo vya habari.
Kova alisema kuwa
maandalizi mengine yanaendelea vizuri
ambapo, hata suala la
viingilio nalo tayari limeshapangwa.
Alisema katika
viingilio vitakuwa vya aina mbili ambavyo ni
sh.20,000 kwa VIP na
kawaida itakuwa sh.10,000.
Alisema kuwa katika
pambano hilo kutakuwa na mapambano ya
utangulizi ambayo
atayatangaza kesho katika mkutano maalum na vyombo vya habari.
Pia Kova alisema
maandalizi yanakwenda vizuri na
kusisitiza kuwa litasimamiwa na chama cha
ngumi za kulipwa Tanzania (PST).
kusisitiza kuwa litasimamiwa na chama cha
ngumi za kulipwa Tanzania (PST).
"Mabondia wote
wako katika hali nzuri ya ushindani, tunategemea Miyeyusho atafanya vizuri na
kukabiliana na upinzani wa mpinzani wake kwani ni bondia mzuri na mwenye
kiwango cha juu," alisema Kova.
0 comments:
Post a Comment