Serikali hoi kwa Majangili - Tembo 39 waua kati ya Januari hadi Machi.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu.
Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema mizoga ya tembo 39 ilionekana ndani na nje ya Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba nchini katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, jijini hapa jana, Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa wizara hiyo, Ibrahim Musa, alisema katika kipindi hicho meno mazima 171 na vipande 22 vya meno ya tembo ghafi, vipande 302 vya meno ya tembo yaliyochakatwa yenye jumla ya kilo 662.62 yalikamatwa.
Pia alisema katika kipindi hicho jumla ya kilo 1,111 za nyamapori za wanyama mbalimbali zilikamatwa.
Alisema bunduki moja ya rashasha, rifle tatu, shotgun mbili, gobori tano na jumla ya risasi saba za aina mbalimbali zilikamatwa.
Alitaja mali na vifaa vingine vilivyokamatwa kuwa ni pamoja na magari matano yaliyohusika katika ujangili hasa wa meno ya tembo.
Aidha alisema ng¡¯ombe 2,663, msumeno mmoja na mbao 745.
Alisema jumla ya kesi 124 zenye jumla ya watuhumiwa 544 waliojihusisha na vitendo vya ujangili zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini na kwamba kati ya hizo, kesi 38 zenye jumla ya watuhumiwa 113 zinaendelea mahakamani na kesi 62 zenye jumla ya watuhumiwa 85 ziliisha kwa watuhumiwa kulipa faini ya jumla ya Sh. Milioni 25, 510,000.
Hata hivyo, alisema takwimu za ujangili katika kipindi hicho ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2014 zinaonyesha kupungua kwa vitendo vya ujangili kwa asilimia 58, isipokuwa kwa idadi ya meno ya tembo yanayokamatwa ambayo yanaongezeka kutokana na kukamatwa meno yaliwindwa siku za nyuma.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:
Post a Comment