NAPE NNAUYE.
Na Florence Sanawa, Mtwara.
OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara imekunjua kucha na kutangaza
kutofanyika kwa mkutano wa hadhara wa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye.
Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kuzuia
mikutano ya hadhara kutokana na vurugu zilizotokea mkoani humo kupinga
ujenzi wa bomba la gesi.
Akizungumza na wana CCM mkoani hapa baada ya kupokea barua ya kuzuiwa
kufungua matawi na mkutano wa hadhara, Nape alisema sasa umefika wakati
kwa Serikali kuangalia sheria na zuio hilo na kwa kina.
Alisema sheria hiyo pamoja na kutungwa na Serikali ya CCM, lakini bado
haiendi na wakati, ikiwemo kuwazuia viongozi kuwafikia wananchi na
kusikiliza kero zao.
“Ni kweli ilikuwa twende kuzindua mashina kwenye maeneo yenu, lakini
liko agizo la Serikali ya CCM, kupitia kwenu hatuoni haja ya kuendelea
na sheria hii, iko haja ya kufungua mikutano iruhusiwe ili demokrasia
zizidi kumea.
“Kwa mtazamo wangu sheria hii inabaka demokrasia, lazima demokrasia
isibakwe hata kidogo, kama hali ni mbaya ni wajibu kwa Serikali kulinda
raia na mali zao na hiyo ndiyo kazi yao, badala ya kuwazuia watu kufanya
shughuli za kisiasa,” alisema Nape.
Katibu huyo wa NEC, Itikadi na Uenezi, alisema CCM ndiyo yenye Serikali
ambapo aliahidi kwenda kushauriana na viongozi ili kuona namna ya
kuondoa zuio hilo.
“Nakwenda kushauriana na serikali na sioni namna ambayo masikio
yatavuka kichwa, tutakubaliana shughuli za kisiasa zitafunguliwa na
mambo yaende vizuri,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, Nape alilazimika kuzungumza na viongozi wa chama
hicho katika ukumbi wa mikutano wa CCM Wilaya ya Mtwara, ambako
aliwataka kuhakikisha wanasimamia uhai wa chama katika maeneo yao
sambamba na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.
Katika kikao hicho cha ndani, Nape alikabidhi bendera kwa viongozi wa
mashina, pikipiki tatu kwa vikundi vya Pentekoste na Jionee zilizotolewa
na Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnen Murji (CCM).MTANZANIA
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment