Mwanza.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Bugando (Cuhas), Musa Mdede ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha Juni 17, mwaka huu bado hatambui alikuwa wapi.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Bugando (Cuhas), Musa Mdede ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha Juni 17, mwaka huu bado hatambui alikuwa wapi.
Kiongozi huyo wa wanafunzi ambaye aliokotwa na wasamaria, amewekwa kwenye ulinzi maalumu na familia yake.
Makamu wa Rais Cuhas, Atukuzwe Mordecai alisema
bado Mdede hatambui alikokuwa licha ya kukumbuka kwamba siku moja kabla
ya kupotea alikwenda Dar es Salaam kwenye kikao cha Umoja wa Wanafunzi
wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso).
Mordecai alisema kutokana na hilo, walishauriwa
kumweka kwenye uangalizi maalumu kwa kushirikiana na familia yake na
kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kwenda kumwona.
“Mdede kwa sasa yupo kwenye uangalizi hadi hapo atakapokuwa na kumbukumbu,” alisema Mordecai na kuongeza:
“Kuna watu wengi wanataka kumwona na kuzungumza
naye, lakini kwa jinsi alivyo sasa hawezi kuzungumza kitu chochote hadi
hapo atakapokuwa na kumbukumbu vizuri, kwani kwa sasa hatambui kitu gani
kilitokea.”
Mmoja wa ndugu zake, Chenga Gudluck alisema kwa sasa hali yake inaendelea vyema licha ya kukosa kumbukumbu.
“Kiafya yupo vyema, lakini mpaka sasa bado hana
kumbukumbu alikuwa wapi. Kiusalama tumeshauriwa akae sehemu maalumu
ambayo atakuwa yeye tu na watu wake wa karibu,” alisema.
Akizungumza kwa simu jana, Naibu Makamu Mkuu wa
Chuo hicho, Ephren Malley alisema uongozi wa chuo hauna cha kusema hadi
polisi watakapomaliza uchunguzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino
Mlowola alisema bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini alipotea
katika mazingira gani.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment