BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWENGE WA UHURU 2014 NAMNA ILIVYOZINDUA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MOROGORO VIJIJINI.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka kushoto akimkabidhi mwenge wa UHURU 2014 mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi baada ya kumaliza mbio zake katika wilaya ya Mvomero na kuzindua miradi ya maendeleo katika makabidhiano yaliyofanyika eneo la Pangawe katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini ambapo Mbio za mwenge wa uhuru 2014 zikiwa na kauli mbiu ya Katiba ni Sheria kuu ya Nchi. PICHA/MTANDA BLOG.

Kataa ukimwi, Malaria, Rushwa na Dawa za Kulevya ni moja ya ujumbe uliobebwa na mwenge wa uhuru 2014 ambapo wakimbiza mwenge huzungumza juu ya adhari ya maneno hayo.
Mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro Sadik Tindwa akikabidhiwa mwenge wa uhuru na mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa Hassan Salum mara baada ya makabidhiano.PICHA/MTANDA BLOG
Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeris naye akikabidhiwa mwenge huyo muda mfupi kabla ya kukimbizwa katika jimbo lake lililopo katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro. PICHA/MTANDA BLOG
Hawa ni skauti wakiwa katika mstari wa wakisuburi mwenge huyo.
Huyu ni mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka akionyesha ukakamavu muda mfupi kabla ya kukabidhi mwenge wa uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini.
Mbikiza mwenge wa uhuru kitaifa, Yusuph Athuman Shesha sambamba na DC wa Mvomero Mtaka na askari wakielekea kukabidhi mwenge wa uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini baada ya kumaliza mbio zake wilaya ya Mvomero. PICHA/MTANDA BLOG
Sehemu ya viongozu wa ngazi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeris wa pili kutoka kushoto, Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Magharibi Dk Rucy Nkya, Mwenyekiti wa CCM Morogoro Vijijini Salum Jazza na DC Said Amanzi kulia
DC Amanzi akisalimiana na mmoja wa wakizmbiza mwenge wa uhuru 2014, Wito Jaston Mlemelwa. PICHA/MTANDA BLOG
 Safu ya viongozi mbalimbali wa kamati ya ulinzi halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi wa sita kutoka kulia wakati wakisuburi kupokea mwenge wa uhuru kutoka wilaya ya Mvomero chini ya mkuu wa wilaya hiyo Anthony Mtaka.PICHA/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: