BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIRI NZITO JUU YA BIDHAA ZA WAMACHINGA KUKAMATWA WAKATI WA OPERESHEMI YAFICHUKA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Mwenyekiti wa Operesheni ya kuwaondoa Wamachinga barabarani jijini hapa, Msongoro Songoro, alisema wapo wafanyabiashara wa aina mbili ambao wanalengwa katika zoezi hilo la safisha jiji; wanaotoa bidhaa ndani ya maduka na kuzipanga nje na wale wanaoweka barabarani.

Katika eneo la mnada wa kuuza vitu vya machinga vilivyokamatwa lililopo katika Soko la Kibasila Gerezani, kulikuwa na makundi ya watu wa aina mbili; waliokwenda kununua vitu vingi kwa bei ndogo na wengine ni wale ambao bidhaa zao ndizo zilikuwa zinapigwa mnada na hawakuwa na uwezo wa kushinikiza wauziwe wao.
Wafanyabiashara waliokuwapo katika eneo hilo jana, walisikika wakisema wamekwenda kununua vitu vya dhuluma na kwamba walilazimika kununua kwa kuwa hakukuwa na njia nyingine ya kufanya.


Leonard Mwagike alisema baada ya bidhaa zake kukamatwa alijaribu kwenda kuzikomboa lakini alishindwa baada ya Mahakama ya Jiji kumwamuru alipe faini ya Sh400,000.


“Kinachoendelea hapa ni dhuluma tu, haiwezekani mzigo wangu wa Sh50,000 uniambie nilipe faini ya Sh400, 000, bora kuja hapa kuununua tena kama nitaweza,” alisema kwa huzuni.


Mfanyakazi wa kampuni moja ya udalali jijini, iliyopewa mamlaka ya kuuza bidhaa hizo, alikuwa akifungua mzigo mmoja baada ya mwingine na kuwataka wafanyabiashara hao wapange bei.


Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, alionekana kutaka kuchukua kila bidhaa aliyoiona ni nzuri, huku akiwaambia wanunuzi kuwa alikwishaichunguza mizigo hiyo kwa hiyo anajua upi ni mzuri.


Mzigo wa kwanza kufunguliwa ulikuwa una vyombo vya plastiki vya kuwekea chakula, ambavyo vyote viliuzwa kwa Sh10, 000. Zilifuata nguo za watoto na chupa za chai, kisha ukafika wakati ulioleta msuguano kiasi cha kutishia mnada kuvunjika.


“Sasa kwenye mzigo huu kuna mali nzuri wengine wameshaiona si ndiyo? Eeh! Ni madera (magauni), mfuko mzima shilingi ngapi?” Anauliza dalali, lakini kabla hajapata jibu anasema:


“Jamani yupo shemeji yenu (mke wake) lazima naye apate hizi nguo (huku minong’ono ikianza kusikika anachukua magauni matatu na kuyaweka pembeni).”


Kitendo hicho kiliwakasirisha baadhi ya machinga waliokuwapo katika eneo hilo, huku wakisema iwapo angeuona mapema mzigo huo angeuchukua wote.


“Mali mmetunyanganya sisi na hata tunazonunua hapa mtazichukua tena, halafu bado mnachukua hata mnazouza, hili halikubaliki,” alisema mfanyabiashara mmoja.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: