BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SAFARI YA MWISHO YA MATESO YA DUNIANI KWA MTOTO NASRA ALIYEISHI KATIKA BOKSI KWA MIAKA MINNE NDANI YA NYUMBA YA MAMA YAKE MKUBWA HATIMAYE AZIKWA NA UMATI WA WATU MOROGORO.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera (mwenye kaunda suti) akimsikiliza Kaimu sheikhe mkuu wa Bakwata mkoa wa Morogoro Ally Mohamed mara baada ya kumalizika kwa shughuli za mazishi za mtoto Nasra aliyeishi katika boksi kwa kipindi cha miaka minne Manispaa ya Morogoro, kwanza kushoto ni Omari Al Saed aliyejitokeza kughalamia shughuli ya mazishi na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro Fikiri Juma .PICHA/MTANDA BLOG


Shughuli za mazishi zilisimamiwa na serikali chini ya ustawi wa jamii ambapo mtoto huyo alifariki dunia juni mosi mwaka huu hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akitibiwa magonjwa mbalimbali akitokea hospitali ya mkoa wa Morogoro ikiwa ni baada ya kufichuliwa na majirani juu ya mateso ya kuishi katika boksi kwa mama yake mkubwa kufuati kifo cha mama yake mzazi kufariki dunia.

Picha zaidi za tukio hilo zitawajia punde kuanzia katika msikiti kuu wa mkoa wa Morogoro wakati wa iabada ya kumswalia, uwanja wa jamhuri wakati wa kuaga mwili wake kisha zile za mazishi katika makaburi ya Kolla mkoani Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: