Wanariadha wanaume wamekiri kuanza kunywa maziwa ya
Matiti kama njia ya kusisimua misuli yao badala ya kutumia madawa
yaliyoharamishwa ambayo yanaongeza nguvu mwili.
Mwanariadha mmoja kutoka mjini New York kwa jina Antony, aliambia jarida la NYMag.com kwamba hukutana na wanariadha kadhaa ambao hunywa maziwa hayo ambayo wanasema ni mazuri na yanawapa nguvu.
Maziwa haya hununuliwa kwenye maduka ya mitandaoni ikiwemo mtandao ujulikanao kama 'Only the Breast and Human Milk 4 Human Babies' kwa dola mbini na nusu.
Mwanariadha huyo anasema kuwa maziwa hayo humpa nguvu za ajabu.
Sababu ya wao kufanya hivyo , ni kujizuia kutumia madawa ambayo yamepigwa marufuku kwani wanaamini kuwa maziwa ya Matiti ni njia ya kiasili ya kuwapa nguvu.
Mwanariadha mmoja ambaye ni baba wa watoto wanne Jason Nash, anasema alianza kunywa maziwa ya mkewe baada ya mtoto wao wa kwanza kuzaliwa na akahisi kuwa ikiwa maziwa hayo ni mazuri kwa mtoto basi pia ni mazuri kwa watu wazima.
Ananukuliwa akisema kuwa maziwa hayo yamemlinda kutokana na magonjwa miaka hii yote.
Wanaume kadhaa wamezungumzia kunywa maziwa ya Matiti kama njia ya kuwapa nguvu badala ya kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Wanaume wengine ambao sio wanaridaha ingawa wanakunywa maziwa ya Matit, wanasema kuwa maziwa hayo huwafanya kujisikia kama walio na nguvu mno na wenye afya tele.
David,mwenye umri wa miaka 42, kutoka Brooklyn, aliambia jarida hilo kuwa alianza kunywa maziwa ya matiti miaka mitatu iliyopita.
Alisema ilisabidia sana wakati alipokuwa anapokea matibabu ya Saratani kwa kuwa alikuwa anahisi kutapika wakati wote alipokuwa anapokea matibabu.
Pindi alipokunywa maziwa hayo hisia za kutapika wakati wote zilimtoka na kusema maziwa hayo ambayo ni matamu , yalimsaidia sana.BBC
0 comments:
Post a Comment