BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TFF YAELEZEA MIKAKATI YAKE KATIKA BUNGE MJINI DODOMA.


http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/03/Nembo-ya-TFF1.jpg
Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukiongozwa na Jamal Malinzi juzi (Juni 21 mwaka huu) mjini Dodoma umekutana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Mtanda (Mbunge wa Mchunga).


Katika kikao hicho TFF ilielezea mikakati yake ya maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Msumbiji.



TFF iliiahidi Kamati ya Bunge kuwa itaendelea kuwa inafanya shughuli zake kwa karibu na Serikali na kamati hiyo ya Bunge.



Katika kikao hicho, ujumbe wa benki ya CRDB ukiongozwa na Meneja wa Electronic Banking, Bw. Mangire Kibanda ulihudhuria ili kutoa ufafanuzi juu ya mradi wa kuuza tiketi za elektroniki, mradi ambao maandalizi yanaendelea vizuri.
 

Bottom of Form

BONIFACE WAMBURA.
OFISA HABARI NA MAWASILIANO.
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: