WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA, NASRA RASHID MVUNGI AKUMBUKWA KWA MATESO YAKE.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaolelewa katika vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa maandamano katika barabara kuu ya Old Dar es Salaam eneo la TRA wakielekea katika viwanja vya shule ya msingi Mwere Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
Katika maandamano hayo Mtoto Nasra Rashid aliyefariki dunia hivi karibuni baada ya kuishi katika boksi kwa zaidi ya miaka mitatu alikuwa akitajwa kwa nyimbo kutokana na mateso yaliyofanywa na walezi wake Manispaa ya Morogoro.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Juma Nondo kulia akiwa amempaka mmoja wa watoto mapacha wa mwanamke aliyejifungua watoto hao, Zuhura Saidi (21) wa pili kutoka kulia huku pacha mwingine akiwa amepakatwa na Tullyesther Mwambapa katika wodi ya wazazi ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika iliyoadhimshiwa mkoani Morogoro, kushoto aliyesimama ni mganga mfawidhi hospitali hiyo Dk Ritha Lyamuya.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Juma Nondo akimvalisha kitenge mkazi wa Kiroka, Husna Salum huku mtoto wake Erisha Steven anayesumbuliwa na ugonjwa wa malaria wodi no 6 akiangalia wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika iliyoadhimshwa kwa kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali katika hospitali ya Morogoro.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto iliyofaanyika Morogoro hoteli iliyoandaliwa na CRDB.
0 comments:
Post a Comment